Tuesday, January 11, 2011

Tukopamoja’ sambamba na kuangusha shoo kali ndani ya ukumbi wa Kimataifa wa Club Bilicanas Januari 16

BAADA ya ziara ya kimuziki bara la Ulaya na Afrika, msanii nyota wa miondoko ya RnB na Bongo fleva nchini, Herry  Sameer 'Mr.Blue' ama kabaisa anatarajia kuzindua video yake mpya ya .
Akizungumza na blog hili jana Mr.Blue ama Kabaisa alisema kuwa katika shoo hiyo ndani ya Bilz atafanya kweli ilikurudisha heshma aliyojijengea kwa mashabiki wake kwa kipindi kirefu. "Mimi sisemi sana, ila watu waje waone wenyewe mimi ndio 'Kabaisa'" alisema Mr.Blue.
Katika shoo hiyo, Mr. Blue atakonga nyoyo vibao vyake vyote vilivyo katika albam zake mbili zikiwemo za 'Mr.Blue' na 'Yote Heri'  huku akitarajiwa kusindikizwa na kundi la B.O.B na  Micharazo, makundi ambayo yanaongoza kwa kudansi na kupafom kwa shoo ya live.
Mr. blue aliongeza kuwa,nyimbo za 'Tabasamu', 'Mapozi' na 'naniumiza' ataziimba kwa ustadi mkubwa sambamba na nyimbo zake mpya ambazo atazifanya 'surprise' kwa washabiki wake ikiwemo kuwaonjesha vionjo na 'lufestyle'.
Mr. Blue mara atapiga shoo hiyo ndani ya Bilicanas hii itakuwa ni ya kipekee kwani mara ya mwisho alipiga miaka saba iliyopita ndani ya ukumbi huo, huku video ya nyimbo yake ya 'Mapozi' iliyotamba katika chati za Bongo nchini aliifanyia ndani ya ukumbi huo kipindi hicho.
 

No comments:

Post a Comment

here u,re comments/acha ujumbe wako hapa