hii hapo juu ni jahazi, mara nyingi hutumika kwa ajili ya kusafirishia mizigo kati ya Mafia na Bara (kisiju - mkuranga) pamoja na visiwa vya Zanzibar. lakini pia wenyeji hutumia huu usafiri kwasababu ya unafuu wa nauli 
 hapo juu ni wafanyakazi wakiwa katika majukumu yao ya kila siku wakiwa katika boti toka kisiwa kimoja kwenda kingine, wakienda fanya usimamizi shirikishi katika vituo vya afya vilivyopo katika visiwa vingine mbali na kisiwa kikuu MAFIA - KILINDONI 
 ukiwa unakuja na usafiri wa ndege hivi ndivyo kisiwa cha MAFIA kinavyoonekana kwa juu, minazi kwa wingi ukizingatia MAFIA ndio wazalishaji wakuu wa MBATA 
  
 hili ni moja ya eneo wenyeju huita jangwa, hapa maji ya bahari huingia nchi kavu wakati wa bamvua (kujaa kwa maji baharini). hapa ndipo kampuni ya uzalishaji wa prawns ilipo ila katika picha haionekekani
ukija MAFIA unaweza tumia chombo kama iki kwa ajili ya utaliii baharini. ahsante karibuni MAFIA
 
No comments:
Post a Comment
here u,re comments/acha ujumbe wako hapa