Wednesday, December 29, 2010

UHALIFU MTANDAO UNAOWEZA KUONGEZEKA MWAKA 2011


Nashukuru mungu kwa kuendelea kuwa mzima mpaka saa hii , saa hii na tarehe kama ya leo niliandika toleo la kwanza la aina za uhalifu ambao ungeweza kutokea mwaka 2010 tumeona karibu yote niliyoelezea mwaka 2009 yametokea lakini kwa kiasi kikubwa na kidogo kutokana na maeneo .
Uhalifu uliohusisha mtandao kwa mwaka 2010 ulitegemeana haswa na uelewa mdogo wa baadhi ya watu wanaofanya kazi kwenye vitengo kadhaa vinavyohusisha mawasiliano na baadhi ya serikali na mashirika ya umma kupuuza ushauri na kutotaka kutumia wataalamu kwenye vitengo kadhaa haswa vinavyohusiana na ulinzi na usalama lakini kwenye sekta ya fedha haswa benki mara nyingi inahusisha zaidi wafanyakazi wenyewe kwa wenyewe .


Mfano hili la mtandao wa WIKILEAKS kuvujisha siri na taarifa za siri za baadhi ya nchi imeleta changamoto mpya katika ulingo mzima wa uhifadhi wa taarifa za siri kwa baadhi ya mashirika duniani hata hapa kwetu kuna siri nyingi zinavuja wakati mwingine kwa makusudi kwa njia ya mtandao na inakuwa ngumu sana kuanzia kufuatilia kidogo kidogo .
Mfano wa pili ni shambulio kwa njia ya mtandao kwa tovuti za wizara ya mambo ya nje ya marekani pamoja na korea kusini mwanzoni mwa mwaka huu matukio kama haya jinsi yanavyofanyika na uharibifu unaofanyika ni mpya kwa dunia ya leo .


Na mfano wa tatu ni jinsi serikali uchina inavyodhibiti na kuchuja taarifa zinazoingia na kutoka nchi hiyo kwa njia ya mtandao lakini hapo hapo ikihusishwa na uvamizi kwenye tovuti za mataifa mengine duniani .


Leo naendeleza mada ya uhalifu unaoweza kutokea mwaka 2011 lakini kumbuka haya ni maoni yangu binafsi na ukitaka taarifa zaidi unaweza kutafuta kwenye mitandao kadhaa vitabu na sehemu zingine kwa ajili ya kujifunza zaidi vile nitakavyoandika .


HARAKATI MTANDAO
Watu kadhaa duniani wanajiuliza kama kitendo alichofanya Assange wa wikileaks ni uhanakarakati au mapinduzi uhuru wa kutoa habari duniani .
Hili tutajadili siku nyingine .


Mwaka huu tulikuwa na uchaguzi mkuu nchini Tanzania tuliona jinsi watu , mashirika na kampuni na vyama vya siasa vilivyotumia teknohama katika kuhabarisha na kuendeleza propaganda kwa ajili ya wagombea mathara yake kwa njia ya mtandao yameonekana wazi haswa kwa kupandikizwa chuki miongoni kwa jamii nchini na aina Fulani za ubaguzi , mara nyingine harakati kwa njia ya mtandao zinaweza kuleta hofu na uwongo kwa watu ili mradi kundi lile lipate linachokitaka .


Ukiacha uchaguzi wetu nchini irani serikali ya nchi hiyo imewahi kutengeneza tovuti kadhaa za jamii kwa ajili ya kupambana kwa kutoa taarifa na propaganda dhidi ya mataifa mengine na wakati mwingine kufunga kabisa mitandao ya mataifa mengine kuweza kuonekana nchini humo au kuchuja kama uchina .


MFUMO CLOUD
Kama mnavyojua mfumo huu kwa sasa umekuja juu sana serikali , mashirika na jamii nyingi zinakimbilia huko katika kuhifadhi vitu na kufanya shuguli zao zingine , vitu hivi na kazi zinahifadhiwa na kampuni maalumu zenye huduma hizo sehemu mbalimbali duniani watu wajiandae kwa aina mpya ya uhalifu kwa njia hii haswa pale ambapo mtu atahifadhi taarifa zake na zikaweza kuingiliwa na wahalifu au anapohifadhi taarifa zake toka kampuni ambayo ni ya kuhalifu pia



Mfano wa ukweli ni Kazi inayofanywa na Mtandao wa WIKILEAKS kwa siku za karibuni hiyo ni moja ya athari za mfumo cloud pale inapohusisha watu kadhaa kuweza kuangalia taarifa na mawasiliano toka upande wowote wa dunia .


ANTIVIRUS,INTERNET SECURITY,FIREWALL
Kuanzia mwaka kesho na kuendelea wahalifu wa mtandao wataingiza na kutengeneza program nyingi za bandia za masuala ya ulinzi na usalama kama antivirus , internet security na firewall kwa ajili ya kuwalaghai watu ili waweze kuibiwa taarifa zao pamoja na hayo ni ile hali ya kuredirect baadhi ya program ziweze kuchota updates toka mitandao ya kuhalifu lakini hii mara nyingi inategemeana na jinsi program hiyo ilivyopatikana kama ni njia halali au bandia hii ni kwa kununua dukani au kwa mtandao au kwa kushusha toka kwenye tovuti zingine ulimwenguni .


Mfano halisi ni jinsi wahalifu walivyojaribu kubadilisha mfumo wa Updates kwa program ya AVG 9 kwenda kuchota update kwenye mitandao ya kihalifu ambapo ilichota virus na aina nyingine ya program za kihalifu .
Tatizo hili haliwezi kuisha kiurahisi kama watu wasipokubali kujifunza na kuzoea bidhaa wanazotumia .


ALL IN ONE
Kwa kipindi cha karibuni kumekuwa na kampuni zinazotengeneza program zinazoweza kufanya kazi nyingi kwa wakati mmoja kuna baadhi ya antivirus zenye uwezo huo na hata Baadhi ya Antispyware kama Adaware wahalifu wanaweza kutumia nafasi hii ya kuunganisha programu bandia kwa ajili ya uhalifu dhidi ya makundi mengine ya watumiaji wa mitandao duniani kwa sababu wengine wanaweza kudanganyika na uwezo wa bidhaa fulani kufanya kazi kwa muda mfupi na kufanya shuguli nyingi .


Hii pia inahusiana na wale watu wanaopenda kuweka taarifa zao kwenye simu za kisasa zilizounganishwa na mtandao moja kwa moja na baadhi ya program zake kwenye komputa kama ni kazini au majumbani mara nyingi kama ni simu ukipoteza simu inawezekana mhalifu akatumia taarifa za simu kuweza kuendeleza mengine ndani ya mtandao .


MITANDAO JAMII
Wakati miaka ya nyuma kidogo wahalifu wengi walitegemea kupata taarifa za wahanga wao kutumia barua pepe kwa sasa wengi wamehamia kwenye mitandao jamii ambapo wanaweza kuomba urafiki na aina nyingine ya ushirikiano na watu wengine waliopo sehemu kadhaa duniani.
Siku hizi ukipita mitaani kwa baadhi ya jamii unakuta kila kijana ametengeneza kurasa yake kwenye mtandao mmoja wa jamii haswa FACEBOOK na mengine iliyojaa duniani watu wengi wanawasiliana na watu wasiowajua mafataki wengi wamejaa kwenye mitandao hii kwa sasa watoto wengi wakike wamelaghaiwa kutumia mitandao hii ni vizuri wazazi majumbani na mashuleni watoe masomo maalumu kuhusu mitandao jamii kwa watoto wao haswa wale ambao ni wageni kwenye mitandao hii na huko tunapoenda uhalifu huu utaendelea kuongezeka na kufikia mahali pabaya .


Kuna watu wengi sana wameweka taarifa zao binafsi kwenye mitandao hii na wengi wao hawajui watoeje taarifa hizo kwa sababu huwa zinatumiwa na wahalifu.


Pamoja na hayo kampuni kadhaa zimetumia mitandao hii kwa kutangaza bidhaa na huduma zao na kupata mafanikio makubwa lakini wengine wametumia mitandao hii kutangaza bidhaa bandia na kampuni au bidhaa ambazo hazipo .


TAARIFA ZA SIRI NA BINAFSI
Huko tunapoenda biashara ya kuuza na kutoa taarifa za siri na binafsi za baadhi ya watu ulimwenguni na kampuni au mashirika inaweza kukua kwa kasi kutokana na taarifa hizo kuibiwa au kuchukuliwa toka sehemu zingine mfano mzuri ni wa tovuti ya wikileaks hizo taarifa zingekuwa zinauzwa watu wengi sana wangenunua , ingawa kuna tovuti kadhaa zinazotoa taarifa za wengine haswa kwa nchi zilizoendelea kwa kiasi cha pesa .


TEKNOHAMA NA MAZINGIRA
Kuna tatizo kubwa kwa sasa haswa kwa nchi zinazoendelea kwenye utunzaji na uharibifu wa vifaa vinavyotumika kwenye teknohama jamii nyingi hazijawekeza sana katika kuelimisha watu kuhusu uhifadhi mzuri wa vifaa hivi kama ni vizima au vibovu , vifaa hivi haswa vilivyotumika vinaendelea kujaa kwenye masoko ya nchi masikini kama Tanzania .


KUJIFICHA , UTUMIAJI WA MAJINA BANDIA


Watu wengi kwenye mitandao bado hawajawa na imani sana na usalama wao pindi wanapojishugulisha na vitu kadhaa haswa zile za utoaji taarifa au ushiriki wa mijadala mengine matokeo yake ni kukua kwa kasi kwa mitandao inayoruhusu watu kutumia majina bandia lakini vile vile mitandao hii mingi inanufaisha watu wachache kimapato zaidi – tatizo hili linaendelea kufanyiwa kazi maeneo kadhaa ulimwenguni ili watu waweze kujiamini na kuweza kushiriki katika kutoa habari na maoni kwa mtandao kwa majini yao na wakiwa huru



Kwa kumalizia tu mwanga wa mafanikio kwenye teknohama kwenye nchi nyingi duniani haswa zinazoendelea ni mzuri sana kwa sasa lakini pia wahalifu wanazidi kuongezeka na wanazodi kuja na njia nyingi za kutekeleza mambo yao ni vizuri serikali na jamii ziwekeze sana kwenye mifumo imara pamoja na kuelimisha umma .


Teknohama imerahisisha sana maisha yetu na uwezo wa watu wengi katika kufanya kazi ulimwenguni ni bora tutumie nafasi zilizopo kwa ajili ya maendeleo ya jamii zetu na mawasiliano pia .


YONA F MARO
WWW.ICTPUB.BLOGSPOT.COM

--
To post to this group, send email to afrojobs@googlegroups.com
 
For International Jobs Visit www.naombakazi.com
For Jobs in Africa Visit http://afrijobs.blogspot.com/


No comments:

Post a Comment

here u,re comments/acha ujumbe wako hapa