Kampuni ya Cross Country Agencies Limited inapenda kutangaza nafasi ya kazi ya
Meneja wa Shamba katika mashamba yake yaliyoko Bagamoyo, Morogoro na Iringa kwa yeyote mwenya sifa zifuatazo:
Sifa
- Awe amehitimu mafunzo katika chuo chochote cha kilimo kilichosajiliwa na kutambuliwa na serikali
.
- Awe na uzoefu wa kazi za kilimo usiopungua miaka mitano (5)
- Awe mtaalamu wa kujua nyakati na majira muafaka kwa kilimo
- Awe tayari kuishi maeneo ya shamba
- Awe mchapakazi, mwaminifu na aweze kukabiliana na changamoto mbalimbali atakazokutana nazo katika utendaji wake.
Kazi zake
1. Kutoa maelekezo ya kitaalamu kwa vibarua pamoja na wafanyakazi wengine wa shamba
2. Kuandaa bajeti ya mwaka, ratiba na mpangilio mzima wa kazi zenye mafanikio.
3. Kutunga kanuni, taratibu na sheria nzuri za uendeshaji wa shamba na kuhakikisha kuwa hazitokwenda kinyume na matakwa ya kampuni.
4. Ataimarisha na kujenga misingi mizuri ya mahusiano ya kibiashara katika masoko aliyoyakuta na atakayoyaanzisha.
5. Atasimamia malipo ya mishahara ya wafanyakazi na vibarua wote na kuandaa ripoti ya siku, wiki ama mwezi Kulingana na makubaliano na kampuni.
6. Atafanya kazi kama Meneja Mwajiri katika:
a) Kuchuja wafanyakazi
b) Kutoa mafunzo ya kilimo kwa wafanyakazi na vibarua
c) Kusimamia sehemu ya kambi, nidhamu na afya za wafanyakazi
d) Kasimamisha ama kufukuza kazi kwa mfanyakazi pale itakapobidi
e) Atawajibika moja kwa moja kukuza ama kuharibu ukuaji wa shamba
7. Kuendesha na kusimamia shughuli zote za shamba kama vile:
Kuandaa shamba, kupanda, kutia mbolea, kuvuna na hatimaye mauzo.
8. Kutoa oda ya vifaa vitakavyohitajika kwa shughuli za shamba, Manunuzi, kutunza na kusimamia matengenezo ya vifaa vilivyoharibika.
9. Atakuwa mfano kwa wafanyakazi kwa kufanya kazi za shamba kwa bidii, na kuonyesha ushirikiano wa bega kwa bega na wafanyakazi wengine.
10. Asiwe muonevu na mbaguzi, aweke wafanyakazi wote katika hali ya usawa ili kuhakikisha kuwa wanakuwa na furaha ili kuleta muamko katika ufanisi wa kazi zao.
Mshahara
Mshahara mzuri na wa kuvutia utakuwepo kwa yule atakayekua tayari kufanya kazi nasi
Jinsi ya kuomba
Barua ya maombi iambatanishwe na :
Maelezo binafsi ya muombaji (CV), Nakala za vyeti, namba ya simu, anuani ya posta na barua pepe pamoja na wadhamini watatu kisha uitume kwa:
GENERAL MANAGER,
CROSS COUNTRY AGENCIES,
P.O.BOX 20651,
DAR ES SALAAM
Barua pepe: info@ljkholdings.com
Mwisho wa kutuma maombi ni Tarehe 30/01/2011
--To post to this group, send email to afrojobs@googlegroups.com
For International Jobs Visit www.naombakazi.com
For Jobs in Africa Visit http://afrijobs.blogspot.com/
No comments:
Post a Comment
here u,re comments/acha ujumbe wako hapa