Translate in your language

Wednesday, September 22, 2010

MUNGU HUMPELEKA MTU KULE ANAKOTAKA KWENDA YEYE

Katika jambo baya kati ya mabaya moja ni kwa binaadam kukosa kujiamini na unapofikiya hapo binaadamu basi jifahamu kama unahitaji msaada wa wengine, maana kutokujiamini kunafuatana sana na uwoga na woga mbaya zaidi ule wa kujitisha mwenyewe maana huu unaweza ukakufikisha pahala wengine wakakuona kama mwendawazimu, na mbaya zaidi hata waliokuzunguka wakijaribu kukuelewesha kwamba huo uliokuwa nao ni woga tu sio uhalisia wewe unabaki kuuwamini ule woga uliojipachika kwamba ndio uhalisiya, na huo uoga humfikisha mtu hata kuamini kinachowezekana yeye akakataa kata kata kwamba hakiwezekani!![kwa kuwa ni muoga tu] wakati  ukweli kischowezekana ni kurudisha uhai tu, na yanayofanywa na binaadamu wengine kwanini wewe ujidharau kusema huwezi wakati nia na nyenzo unazo za kukuwezesha!!
nasikitika sanaaa na nawashangaa hawa ndugu zetu  WAZANZIBARI wenye kuanza  kasumba mabaya na zenye  kutuvunja moyo kwa kututangaziya kwamba zanzibar hatuwezi kufika huko tunakotegemeya tulio wengi, basi hata angalau mfano wa nchi kama Mauritius ambayo ni moja ya nchi zilizopiga hatuwa na ni mfano wa ZANZIBAR na iko ndani ya afrika pia, nawaomba ndugu zangu tuwache kujidharau na kujitisha [lakini yawezekana wengine kati ya hao wanachosema sio wanachokiamni], kwani hao walioweza wamaweza vipi hata sisi tushindwe au wao waloweza walishushwa kutoka mbinguni? tusikatishane tamaa!, muhimu tuwe na nia na ukweli tu SABABU MUNGU HUMPELEKA MTU KULE ANAKOTAKA KWENDA sasa nawaomba  tusiwe  siku zote kutaka kubaki hapa tulipo,
tuamini yote yawezekana kama yalivyowekana na binaadamu kama sisi, ila tukikubali kwamba hayawezekani basi kweli hayatowezekana kamwe..
ZANZIBAR MPYA, MATUMAINI MAPYA, DHAMIRA MPYA..

No comments :

Post a Comment

here u,re comments/acha ujumbe wako hapa

Kijiweni (nipe 5)