Translate in your language
Friday, September 24, 2010
JK aomba kura kwa kukaa chini
MGOMBEA urais kwa tiketi ya CCM, Jakaya Kikwete alitumia staili ya aina yake kuomba kura wakati alipolazimika kuketi ardhini ili kumsikiliza mwananchi wakati akiwa kwenye moja ya mikutano ya kampeni za kuomba kura kabla ya uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika Oktoba 31.
Mbali na tukio hilo, kabla ya kupanda jukwaani mjini Ludewa wilayani Mbalali, Kikwete alikuwa akizungumza na simu na baada ya kumaliza aliwaambia wananchi kuwa alikuwa akizungumza na balozi wa Marekani nchini Tanzania na kwamba balozi huyo amemueleza kuwa Rais Barack Obama ameahidi kuwa serikali yake itaendelea kutoa misaada kwa Tanzania.
Watu wengi hawakuamini macho yao wakati Kikwete alipoanza kukaa chini kwa ajili ya kumsikiliza mwananchi huyo, Sara Mageni kwenye mkutano wake uliofanyika kwenye Uwanja wa Mabehewa wilayani Makete ambako wakati huu wa majira ya kipupwe vumbi limeshamiri.
kwa maelezo zaidi bofya hapa
2 comments :
mh, hivi yeye bado ni rais kwa wakati huu wa kampeni?
mi kwa ufahamu wangu yeye kwa sasa si rahisi kwani nae yu mbioni kugombea, sema ni ufinyu wa katiba yetu ndio maana anaonekana kama bado ni rahisi, nchi ilitakikakana kwa sasa iwe chini ya mwanasheria mkuu wa serikali.
kuwepo kwake kwa sasa wakati wa uchaguzi tunashindwa fahamu maana anashindwa kujitofautisha yeye ni mgombea au raisi
Post a Comment
here u,re comments/acha ujumbe wako hapa