HUKU Serikali ya Tanzania kkwa kushirikiana na jumuiya za taasisi kupambana na magonjwa ya Ukimwi lakini hali imekea tofauti ambapo hapo jana Ofisi ya Serikali ya Mtaa wa Oyster-Bay kwa kushirikiana na kikosoi maalum cha Polisi Jamii kubaini danguro linalotumiwa kwa ajili ya kufanyia biashara ya ngono.
Kubainika kwa danguro hilo la kienyeji ni kufuatia msako mkali uliofanywa na Mwenyekiti wa mtaa huo Peter Mushi kwa kushirikiana na kikosi hicho cha Polisi Jamii kijulikanacho kama ‘Oyster Bay Guard’ ambapo walifanya msako huo mkali nakubaini danguro hilo kubwa linalotumiwa na kwa biashara hiyo ya ngono zembe kwa makahaba hao huku likiwa na uwezo wa kuingiza watu saba kwa wakati mmoja.
Mwenyekiti huyo akiwa ameongozana na waandishi walifika katika eneo hilo ambalo lipo mkabala na ukumbi maalufu wa burudani katika barabara ya Haile Selasie na Quba, huku mmiliki anayelitumia kwa kufanyia biashara ya kupanda na kuuza miche na maua mbalimbali, inadaiwa ameligeuza eneo hilo majirta ya jioni kwa biashara hiyo.
Mushi aliwaelezea waandishi wa habari kuwa, zoezi kubwa lililopo katika mtaa wake huo ni juu ya kuwaondoa wafanyabiashara hao wa ukahaba sambambanakutokomeza uhalifu unaofanywa kwa kuiba kutumia magari.
“Zoezi ili litaendelea siku zote katika maeneio yote ya Oyster-Bay na kwa kuakikishabiashara hii ya ukahaba inaondoka na kuwa historia sambamba nakutokomeza vitendo vyote vya kiharifu maeneo haya ambayo yanaishi viongozi na maofisa wa nchi mbalimbali” alisema.
Kwa upande wake, mmiliki wa eneo hilo,alijitambulisha kwa jina moja la Mwinuko, alikana kwa eneo lake hilo pamoja na mashimo hayo kutumiwa kwa vitendo hivyo vya kikahaba huku akisisitiza kuwa makahaba hao wanapatumia hapo kwa manufaa yao wala yeye ausiki nao.
Eneo hilo ambalo kipindi cha nyuma lilikuwa maalufu kwa biashara hiyo huku makahaba hao wakiwabuguzi baadhi ya viongozi akiwemo kiongozi wa ngazi ya juu Serikalini kusimamishwa na kufanyia fujo katika eneo hilo la Oyster Bay.
No comments:
Post a Comment
here u,re comments/acha ujumbe wako hapa