Tuesday, September 14, 2010

CUF kupunguza idadi ya mawaziri ikiingia Ikulu

CHAMA cha Wananchi (CUF) kimeahidi kuunda Baraza la Mawaziri 19 tu kama kikiingia Ikulu ikiwa ni njia ya kupunguza gharama za Serikali.

Mkurugenzi wa Uhusiano na Siasa wa chama hicho, Mbarala Maharagande alisema hayo juzi alipokuwa akihutubia katika mkutano wa kampeni na kuongeza kuwa fedha zinazotumika sasa kwa mishahara na posho za mawaziri, zitaelekezwa kwenye sekta zingine.

Maharagande alifafanua kuwa serikali yao haitaendekeza maisha ya anasa miongoni mwa mawaziri wake na itaweka bajeti ya kiwango maalumu kwa ajili ya matumizi yao.

“Kwenye serikali yetu, mawaziri watakuwa wakinywa chai nyumbani kwa waume na wake zao, watakuwa wakipewa kiwango maalumu cha fedha katika bajeti yao kwa ajili ya mafuta na kama watashindwa kutumia vizuri watalazimika kutumia usafiri wa jumuiya kwenda na kurudi kazini,” alisema huku akishangiliwa na umati wa watu.
kwa maelezo zaidi bonyeza hapa

No comments:

Post a Comment

here u,re comments/acha ujumbe wako hapa