Wednesday, September 29, 2010

Ajinyonga kwa kuitwa ‘shoga'

Ajinyonga kwa kuitwa ‘shoga'  

MKAZI wa Kinondoni Deogras Paul (39) amekutwa chumbani kwake akiwa amejinyonga kwa kutumia shuka  kwa kile kilichodai kuitwa hanithi ‘shoga’  na majirani zake.
 
Akizumguza na wandishi wa habari leo , Kamanda wa Polisi Mkoa Kinondoni, Elias Kalinga alisema kuwa, tukio hilo lilitokea jana huko maeneo ya Kinondoni majira ya saa moja kasoro robo ya jioni, alikutwa humo akiwa amejinyonga.
 
Kamanda Kalinga alielendelea kusema kuwa, marehemu alikuwa amejinyonga kwa kutumia shuka hiyo aliyoitundika  kwenye dali ya chumba hicho na kupelekea kifo chake hicho, hata hivyo walipopekua walimkuta ameacha ujumbe uliosema kuwa; “Mimi sio shoga, ninafamilia na mtoto, Mungu shahid”, ilieleza maelezo ya ujumbe huo.
 
Mwili wa marehemu umeifadhiwa katika Hospitali ya Mwananyamala na upelelezi juu ya hali hiyo unaendelea.
 
 Katika tukio jingine, msako ulifanywa na jeshi hilo katika mikoa ya Ilala na Temeke, walifanikiwa kukamata watuhumiwa 10,kwa kukamatwa na lita za gongo 16 na Puli mbili za bangi.
 
Watuhumiwa hao ni; Masanja Peter (29) mkazi wa Temeke, wenbgine ni Pascal Jeseph (28), Omary Said (47) Veronica Philipo (22) na wenzao  sita.
 
Mwisho
 
 
Wananchi: Kakobe yupo sahihi
Na Andrew Chale
KUFUATIA kauli ya Askofu Mkuu wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship, Zachary  Kakobe  kuwatangazia waumini wake kuwa hatokuwa na ibada jumapili ya Octoba 31, ilikuwaruhusu kufanya kampeni watu mbalimbali wamesifu na kupongeza huku wengine wakibeza kwa hatua hiyo.
 
Katika uchunguzi uliofanywa na gazeti hili katika maeneo mbalimbali na pamoja na kuojiana na baadhi ya watumishi wa Mungu juu ya uamuzi wa Kakobe wengi walipongeza kwa hatu hiyo huku wengine wakibeza kwa madai mbalimbali.
 
“Kitendo alichokionyesha Kakobe kwa kufuta ibada ni jambo ambalo linatakiwa kuungwa mkono na madhehebu yote nchini ilikuwapa uhuru waumini kumchagua kiongozi ambaye atawafaa” alisema Wilson Jengera ambaye ni muumini wa makanisa la T.A.G ( Tanzania Assembles of God).
 
Kwa upande wake, Samson John(47) licha ya kupongeza uamuzi huo wake huo wa kufuta ibada, lakini ingependeza kama angekuwa amewashirikisha  madhehebu mengine ya kikristo ilikuweza kufanya hilo kwa pamoja.
 
“Ni vizuri  na ameonyesha mfano wa kuigwa kwa hilo , ingekuwa vizuri pia angeshirikisha na wengine ilitujue kama wangekuwa tayari” alisema.
 
Wengine waliiambia Tanzania Daima kuwa, hatua hiyo ya Kakobe ni  ya kuigwa na viongozi wote wa dini ingawa bado nao hawajaonyesha waziwazi kutangaza rasmi.
 
“Jambo hili linaitaji kukubaliana, ikizingatia kila kanisa sasa linapigania kuzoa waumini ilikuwa na wafuasi, aangalie asije kuwapoteza hiyo siku” alisema mmoja wa wananchi ambaye alikataa kutaja kuandika jina lake gazetini .
 
Hata hivyo wengine walibeza hatua hiyo na kudai kuwa amekurupuka kwani mbali na kuwatangazia waumini wake, alitakiwa kuonyesha ni jinsi gani alivokuwa akifanya maswala ya Mungu pasipo kuingiza siasa makanisani.
 
“Hatua yake ni nzuri, lakini kwa kuanza kuongea mambo ambayo yanajadiliwa na wanasiasa kwenye majukwaa, ni kitendo ambacho kinakiuka  misingi sahihi ya kiimani, anatakiwa kusimamia haki ya kiimani pasipo kuchanganya na siasa” alisema mwananchi ambaye naye hakutaka jina lake liandikwe gazetini.
 
Kwa upande wa baadhi ya viongozi wa dini ya kikiristo walipotafutwa kuonyesha msimamo wao juu ya swala hillo, hawakuweza kupatikana kwa huku wengine simu zao zikiita bila kupokelewa.
 

No comments:

Post a Comment

here u,re comments/acha ujumbe wako hapa