MO DEWJI AANZISHA MICHUANIO YA WANAWAKE SINGIDA MJINI
Akizungumza katika hafla fupi ya kukabidhi vifaa kwa timu za Kata 13 za jimbo hilo, Katibu wa Mbunge Hasan Mazala alisema MO ameamua kuanzisha mashindano hayo kwa lengo lakukuza vipaji hasa vya wanawake kupitia mpira wa miguu.
Mazala alisema katika michuano hiyo ya wanawake mshindi wa kwanza atapata kombe pamojana zawadi ambazo hata hivyo hakuweka bayana kwa madai kuwa atazitangaza siku ambayo mashindano hayo yataanza.
Aidha alisema katika michuano hiyo inayotarajiwa kufunguliwa na MO mwenyewe kwenye uwanja huo, amewataka masahabiki kufika kwa wingi ili kushuhudia vipaji vya wanawake wa mkoa wa Singida.
Timu zilizopewa vifaa hivyo ikiwa ni pamoja na jezi mipira na fulana maalumu za washabiki ni Kata za Ipembe, Mughanga, Kindai, Majengo, Utemini, Mitunduruni,Mwankoko, Mungumaji, Unyamikumbi, Unyambwa , Mtamaa na Mtipa
No comments :
Post a Comment
here u,re comments/acha ujumbe wako hapa