Translate in your language

Thursday, June 10, 2010

MO DEWJI AANZISHA MICHUANIO YA WANAWAKE SINGIDA MJINI



Katibu wa Mbunge Hassan Mazala akimkabidhi Mwenyekiti wa chama cha Mpira wa miguu wanawake Mkoa wa Singida (SWFA) Mwanaasha Ramadhani jezi kwa ajili ya kuzigawia kata zitakazoshiriki michuano hiyo.


Kombe linaloshindaniwa.
Mbunge wa jimbo la  Singida Mjini Mohammed Dewji  (MO) ameanzisha mashindano ya mpira wa miguu kwa wanawake wa jimbo hilo. Mashindano hayo ambayo yatajulikana kama (Mohammed Dewji Cup Women Football) yanatarajiwa kuanza kutimua vumbi Jini 11 mwaka huu katika uwanja wa michezo wa Namfua.



Akizungumza katika hafla fupi ya kukabidhi vifaa kwa timu za Kata 13 za jimbo hilo, Katibu  wa Mbunge Hasan Mazala alisema MO ameamua kuanzisha mashindano hayo kwa lengo lakukuza vipaji hasa vya wanawake kupitia mpira wa miguu.
Mazala alisema katika michuano hiyo ya wanawake mshindi wa kwanza atapata kombe pamojana zawadi ambazo hata hivyo hakuweka bayana kwa madai kuwa atazitangaza siku ambayo mashindano hayo yataanza.
Aidha alisema katika michuano hiyo inayotarajiwa kufunguliwa na MO mwenyewe kwenye uwanja  huo, amewataka masahabiki kufika kwa wingi ili kushuhudia vipaji vya wanawake wa mkoa wa Singida.
Timu zilizopewa vifaa hivyo ikiwa ni pamoja na jezi mipira na fulana maalumu za washabiki ni Kata za Ipembe, Mughanga, Kindai, Majengo, Utemini, Mitunduruni,Mwankoko, Mungumaji, Unyamikumbi, Unyambwa , Mtamaa na Mtipa

No comments :

Post a Comment

here u,re comments/acha ujumbe wako hapa

Kijiweni (nipe 5)