Biden akutana na viongozi wa Kenya
Makamu wa rais wa Marekani Joe Biden amekutana na Rais wa Kenya Mwai Kibaki, Waziri Mkuu Raila Odinga na Makamu wa Rais Kalonzo Musyoka katika ikulu ya Rais mjini Nairobi.
Baada ya mazungumzo yao ya faragha viongozi hao walihutubia waandishi wa habari ambapo Bwana Biden amesema Marekani itashirikiana na Kenya katika kukabiliana na hali msukosuko nchini Somalia na Sudan.
Makamu huyo wa rais wa Marekani pia amesema taifa lake linaunga mkono juhudi za Kenya kupata katiba mpya.
Bwana Biden pia amekutana na Mawaziri wa Kenya wa maswala ya kigeni Moses Wetangula, Usalama wa ndani George Saitoti na Mutula Kilonzo wa maswala ya Haki na Katiba. Naibu waziri wa maswala ya kigeni wa Marekani anayehusika na maswala ya Afrika Johnnie Carson pia amehudhuria mkutano huu.
Baadaye Bwana Biden atasafiri kuelekea Afrika Kusini kwa ufunguzi wa dimba la Kombe la Dunia litakaloanza Ijumaa Juni 11.
No comments :
Post a Comment
here u,re comments/acha ujumbe wako hapa