Polisi leo; Mei 30
WATU wawili wamefariki dunia katika matukio tofauti likiwemo la fundi kubanwa na mashine ya kuchang’anyia cement na mwinge kuzama maji katika ufukwe wa bahari ya Hindi.
Katika tikio la fundi ambaye aliyefahamika kwa jina la Mbaraka Mkongame(22) amefariki dunia baada ya kulaluliwa na mashine ya kuchanganyia Cementi.
Akizungumza na waandishi wa Habari jana Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Elias Kalinga alisema kuwa tukio ilo lilitokea juzi majira ya saa moja jioni huko eneo la UFI, Urafiki.
Kalinga alisema marehemu alikumbwa na mauti hayo alipokuwa anachanganya cementi katika mashine hiyo na kuingiza katika bomba, ghafla mkanda wa Ovaroli aliyovaa ilinasa katika mashine hiyo na kumchana utumbo.
“Mashine hiyo ilimchana utumbo na kumlalua hadi utumbo kutoka nje sehemu za kitovu na kupelekea kifo chake hicho” alisema Kalinga.
Hata hivyo baada ya kutokea tukio hilo , walizima mashine hiyo lakini alikuwa tayari ameshapoteza maisha.
Mwili wake umehifadhiwa katika Hospitali ya Mwananyamala na uchunguzi unaendelea.
Katika tukio jingine,Kamanda Kalinga alidai kuwa mtu aliyefahamika kwa jina la Idd Salum (20) alifariki dunia alipokuwa akiogelea katika ufukwe wa bahari ya Hindi eneo la Jangwani Beach .
Kalinga alisema tukio hilo lilitokea juzi majira ya saa 12 jioni, ambapo inadaiwa marehemu alikutwa na mauti hayo baada ya kunywa maji mengi.
Mwili uliopolewa na wananchi waliokuwa jirani na ufukwe huo na kuifadhiwa katika Hospitali ya Mwananyamala.
Aidha, Katika tukio jingine, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, David Msime alisema kuwa huko katik barabara ya Nyerere banda la Ngozi gari lililokuwa na namba T 2119 BCH aina ya Benz likiendeshwa na Naila Kalembo, ghafla liliteketea kwa moto na kuunguza gari lote pamoja na mali zilizokuwemo humo.
Kamanda Msime alisema kuwa gari hilo lilikuwa likitokea maeneo ya Kamata na kuelekea TAZARA, huku chanzo cha ajali hiyo na thamani nzima bado haijafahamika na uchunguzi unaendelea
No comments:
Post a Comment
here u,re comments/acha ujumbe wako hapa