Translate in your language

Tuesday, May 25, 2010






---
WAPIGA KURA NJOMBE WAMCHNGIA MGOMBEA 20,000 ZA KUWANIA UBUNGE


 

WAPIGA  kura wa jimbo la Njombe Magharibi  wamemchagia kiasi cha shilingi 20,000 mbunge wa jimbo  hilo Yono Kevella ili muda ukifika achuku  fomu ya kugombea tena ubunge katika  jimbo  hilo na kumtaka aliyekuwa mbunge wa  jimbo hilo Thomas Nyimbo  kutafuta shughuli nyingine ya kufanya na sio  kurudia  kugombea ubunge kwani kufanya  hivyo ni sawa na kula matapishi yao.

 

Wananchi hao wa kijiji cha Mlevela  kata ya Igima walitoa msimamo  wao huo juzi  katika harambee iliyoendeshwa na mbunge Kevella ambapo pia mbali ya kuanchagi  fedha hizo za kuchukua fomu pia walimuunga mkono katika harambee  hiyo kwa kuchangia zaidi ya shilingi milioni 1 zilizokuwa zikihitajika kwa ajili ya  kukamilisha ujenzi wa kituo cha afya kijijini hapo.

 

 

 Akizungumza baada ya  kumalizika kwa harambee hiyo  kwa niaba ya wakazi wa kijiji  mwenyekiti wa chama cha TLP  jimbo la Njombe Magharibi  Yohana Mgowelo  alisema kuwa  toka  nchi ipate  uhuru wake mwaka 1961 kijiji hicho hakijapata kuwa na kituo  cha afya hali iliyokuwa  ikiwalazimu wagonjwa kutembea  masaa zaidi ya mawili kwenda  kupata  huduma ya afya katika kijiji cha jirani ama katika hospitali ya wilaya ya Njombe.

 

"Mimi hapa ni mwenyekiti wa jimbo  hili la Njombe Magharibi  kupitia chama cha TLP  ….ila ukweli lengo letu wapinzani sio kubeza kila jambo  ….jimbo  hilo huyu ni mbunge wa  pili  kuongoza ambapo mtangulizi wake alikuwa Thomas Nyimbo …lakini maendeleo yaliyopatikana sasa  huwezi linganisha nay ale ya Nyimbo ….sasa kwanini tusimpongeze  hata kwa kutuwezesha kupata huduma hii ya afya hapa…nasema tupo pamoja"alisema kiongozi huyo 

 

Pia alihoji sababu za wabunge wa CCM ambao wamepata kuongoza majimbo na kung'olewa katika nafasi zao  kurudi  kutaka kugombea tena  ubunge    na kuwa ni vema wananachi  kuwa makini na njama chafu  zinazofanywa na chama cha mapinduzi kwa kuendelea  kuwapitisha  wabunge  wale wale miaka yote.

 

Hata hivyo kwa upande wake mbunge  Kevella akiwapongeza wananchi hao kuwa michango yao kwa ajili ya shuguli za kimaendeleo alisema kuwa   jimbo  hilo ni moja kati ya majimbo  yanayo piga hatua kubwa katika maendeleo na kuwa mbali  ya  Manispaa ya Iringa kuwa na idadi kubwa ya vyuo vikuu ila bado wilaya ya Njombe katika  jimbo la Njombe Magharibi ni miongoni mwa wilaya na majimbo  yenye maendeleo makubwa kwa kuanzisha  chuo  kikuu kishiriki cha Tumaini .

 

 

Kevella alisema kuwa  pamoja na kuwa aliyekuwa mbunge wa jimbo  hilo Thomas Nyimbo ameweza kuponda  jitihada za kimaendeleo katika jimbo hilo  ila bado wananchi wana kila  sababu ya  kuwabeza  wale wote  hasa wana CCM wanaotaka  kuwania nafasi mbali mbali za uongozi ambao  wanajitokeza kupinga kazi zilizofanywa na chama hicho .

 

 

Kwani alisema  ni vizuri  kazi ya kupinga ifanywe na wapinzani ila sio  wana CCM na kuwa mwana CCM mwenye tabia kama ya Nyimbo ya kupinga  kazi zilizofanywa na chama   tawala chini ya Rais Jakaya  kikwete  atakuwa amepoteza mwelekeo  wa kuja kuomba kuwatumikia wananchi .

 

Mbunge  huyo alisema kuwa  kutokana na kituo hicho cha afya  kukamilika bila kuwa na kitanda hata kimoja kwa upande wake kama mbunge atajitolea vitanda  vyote katika kituo hicho pamoja na  kununua madawati katika  shule ya awali ya kijiji cha Idunda  ambayo  wanafunzi wake zaidi ya 60 pamoja na walimu wamekuwa wakikaa chini.

 

Wakati huo huo  wana CCM katika kata  hiyo  wamekitaka chama cha mapinduzi (CCM) wilaya ya Njombe  kukemea tabia ya uongo kwa wanachama wanaotaka kuwania ubunge katika jimbo  hilo ambao wamekuwa wakiwasema uongo wabunge na madiwani  wa CCM  huku wakisahau kuwa  kauli zao na uongo zinakiweka pabaya chama hicho na kuonekana vibaya kwa wapinzani  kuwa hakuna jipya ambalo limefanywa kwa kipindi chote cha miaka mitano alisema katibu wa CCM  kitongoji cha Idunda  Ayubu  Mwipela






No comments :

Post a Comment

here u,re comments/acha ujumbe wako hapa

Kijiweni (nipe 5)