SIMBA SC YAKIPIGA NA EL HADOUD
LEO HIIIIII
KIKOSI CHA SIMBA SC 2009/2010..LEO MEI 8 INASHUKA KATIKA DIMBA LA EL MAX
Na Mwanablog wetu
WAWAKILISHI wa
Simba iliwasilili jana mjini
Kwa mujibu wa ofisa habari wa Simba, Cliford Ndimbo, wachezaji wote wako katika hali nzuri na wameahidi kutofanya makosa leo kwa kuhakikisha wanawafunga wapinzani wao na kusonga mbele.
Alisema licha ya kuwa mechi hiyo itakuwa na upinzani mkubwa, uhakika wa kuibuka na ushindi upo na hasa ukizingatia licha ya kujifua pia wamewajenga vema kisaikolojia wachezaji wao.
Katika mechi ya awali iliyopigwa jijini Dar es Salaam wiki mbili zilizopita, Simba ilishinda mabao 2-1, hivyo leo itakuwa ikipigana walau kuvuna sare ili kusonga mbele.
Simba inapaswa kupambana vilivyo hasa ikizingatia iko ugenini huku wapinzani wao wakiwa na bao la ugenini ambalo lilifungwa na Ahmed Eid Abdemalek.
Wakali walioondoka na Simba ni Haruna Shamte, Salum Kanoni, Juma Jabu, Nico Nyagawa, Kelvin Yondan, Juma Nyosso, Mohamed Banka, Ramadhan Chombo, Musa Hassan 'Mgosi', Ulimboka Mwakingwe, David Naftal, Uhuru Seleman, Jerry Santo, Mohamed Kijuso, Emmanuel Okwi, Jabir Aziz na Joseph Owino.
No comments :
Post a Comment
here u,re comments/acha ujumbe wako hapa