Tuesday, May 4, 2010

MAREKANI YATOA FOMU  MPYA ZA DS-160 KWA MATEMBEZI YA MUDA MFUPI

 

 

 

Na Mwanablog wetu

 

UBALOZI wa Marekani Dar es Salaam umeungana na mabalozi mengine duniani kwa kutumia fomu mpya za  DS -160  kwa ajiri ya  maombi ya matembezi ya muda mfupi itakayoanza kutumika  kuanzia  Mei 31 mwaka huu.

 

Katika taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa jana na Ubalozi huo jana jjini Dar es Salaam, ilieleza kuwa, waombaji wote wa matembezi ya muda mfupi watatakiwa kujaza fomu hizo za DS 160 itakayo kuwa ikipatikana katika mtandao huku kila muomba viza anashauriwa kuanza kutumia fomu hiyo mpya bila kuchelewa.

 

Taarifa hiyo ilielezea kuwa; Idara ya Uhamiaji, Wizara ya mambo ya nje Marekani imeboresha DS-160 kwa wale waombaji wote wa aina hiyoo ya muda mfupi (NIV) Fomu hii italeta mabadiliko kwenye fomu zote zinazopatikana kwenye mtandao (EVAF).

 

Mabadiliko ya Viza DS-160,  yataleta mabadiliko kwenye hatua ya kwanza ya maombi pamoja na faida nyingi kwa waombaji wa viza Dar es Salaam ambao tayari wameisha jaza fomu zao kupitia kwenye mtandao'.alieleza taarifa hiyo.

 

Katika fomu hiyo mpya, tofauti yake  ni kwa waombaji kutuma maombi yao kwenye mtandao, huku pia muombaji wa viza anapata fursa ya kuhifadhi fomu zao kwa matumizi ya siku zijazo. Unatakiwa kutuma picha ya mnato, na kama maombi yanakuwa ni ya kundi unashauriwa kutumia fomu itakayokuwa ya vikundi ili kuepuka makosa ambayo yanaweza kujitokeza wakati wa kujaza. DS-160.

 

Kwa hali hiyo, kila mmoja anahitajika kujibu  maswali yote ili kuepusha usumbufu ambao ubalozi itabidi wakurudishe kutokana na kutokamilika kwa fomu zako. Pia watapata kujipangia muda (miadi).

 

Ikifafanua zaidi taarifa hiyo, ilisema uchunguzi uliofanywa na huduma kwa wateja Duniani kote, umeonyesha mafanikio makubwa ya kuridhisha na fomu hiyoo mpya muombaji wa Viza atatakiwa kuleta uthibitisho wa kupokelewa kwa maombi yake Ubalozini wakati wa mahojiano.

 

Mitandao na tovuti ambayo fomu hizo za  DS -160 inapatikana na kupata maelezo ya hatua kwa hatua  ni kupitia ; http://www.tanzania.usembassy.gov ama kutembelea katika ofisi za balozi hizo ama kuwasiliana na idara ya uhamiaji kwa barua pepe drsniv@state.gov.

 

 

Mwisho 


No comments:

Post a Comment

here u,re comments/acha ujumbe wako hapa