Translate in your language

Saturday, May 1, 2010

 

 MAAFA MAKUBWA MAFIA

 

UPEPO MKALI WAHEZUA NYUMBA 53, KAYA 135 ZAKOSA MAKAZI

 

 

Mkuu wa Wilaya Mh. Manzie  Mangochie akiwa na kofia ya njano 

 

 

Na mwanablog wetu Mafia

 

UPEPO mkali umekikumba kisiwa cha Mafia na kuhezua nyumba 53 na kusababisha maafa kwa wakazi wa Kaya 135 kukosa Makazi na wengine saba kujeruhiwa vibaya.

 

Akizungumza na bog hii leo asubuhi Mkuu wa Wilaya ya Mafia, Manzie Mangochie alithibitisha kuwepo kwa tukio hilo lililotokea mwishoni mwa wiki  April 28 majira ya saa nne asubuhi na kupelekea maafa kwa Kaya hizo 135.

 

Mangochie alisema kuwa, upepo huo ulitokea upande wa Kusini kuelekea Magharibi ndio uliothababisha maafa hayo kwa kuhezua mabati ya nyumba hizo takribani 53 pamoja na kuharibu mazao kadhaa ikiwemo minazi.

 

Baada ya kutokea tukio hilo, Mangochie alisema kuwa, ofisi yake iliweza kutoa magari kadhaa ikiwemo ya kubebea wagonjwa na malori ya kuwahamisha kwa muda waanga waliokumbwa na Upepo huo.

 

"Baada ya kutokea kwa  tukio ilo, sote tulifika eneo la tukio na kutoa msaada, kwa kweli lilikuwa la aina yake, napenda kuwatoa hofu wakazi waliokumbwa kuwa, kile sio Kimbunga kama walivyo dhani, bali ni upepo mkali "Cyclone" hivyo wasio hofu Mamlaka ya hali ya hewa wataendelea kurtoa taarifa zaidi juu ya hilo' alisema Mangochie.

 

Mangochie aliyataja maaeneo yaliyokumbwa na Upepo huo kuwa; Kilungeni A, Vunjanazi na Ismailia, ambapo kati ya nyumba hizo 53,  Nyumba 50  ambazo zilikuwa ni makazi ya watu, ofisi mbili na gereji moja.

 

Pia majeruhi waliokumbwa ni pamoja na wanafunzi wanne wa shule ya msingi Kilimahewa Wasichana, walikimbizwa Hospitali na hali zao zinaendelea vizuri na wengine wawili walipatwa mishtuko na mmoja alivunjika mguu baada ya kuangukiwa na tofari.

 

Kisiwa hicho cha Mafia, hali ya hewa ni mvua kali karibu wiki nzima sasa, licha ya kimbunga hicho, pia mvua hiyo inayoendelea kunyesha imesababisha baadhii ya sehemu za mji huo wa Kilindoni maeneo ya Majengo kujaa  mafuriko.

 

Mangochie alisema kujaa kwa maji hayo yaliyosababisha mafuriko, yalitokana na kuziba kwa mifereji mingi katika maeneo kadhaa ya mji huo.

 

Kitokea kwa tukio hilo ambalo lilizua hofu kwa wakazi hao huku wengine wakikimbia pasipojua wanaenda wapi, baadhi ya taarifa kutoka kisiwa hicho zilidai kuwa upepo huo ulikuwa mkali kama kimbunga ambapo ulikuwa ukitembea kwa kasi ukitokea Visiwa vya nchi jirani ya Comoro na kumalizikia katika Kisiwa hicho.

 

 


No comments :

Post a Comment

here u,re comments/acha ujumbe wako hapa

Kijiweni (nipe 5)