KICHANGA CHA SIKU 25 CHATEKETEA KATIKA MOTO
Na Mwanablog wetu Dar
WATOTO wawili wamefariki dunia katika matukio tofauti jijini
Katika tukio la kuteketea kwa kichanga hicho, jana Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, David Msime aliwaambia waandishi wa Habari kuwa ajali hiyo ilitokea majira ya saa moja na nusu usiku huko maeneo ya Ferry Kigamboni baada ya moto kuzuka ghafla kwenye nyumba iliyokuwa na vyumba sita na kuteketeza chumba hicho kimoja alichokuwa kichanga huyo.
Kamanda Msime alieleza kuwa,chumba hicho kilikuwa cha mpangaji ambaye ni mama wa kichanga hicho, Mwantoro Haji (30), ambaye aliwasha kibatari na kutoka kuteka maji nje ya nyumba hiyo., ambapo moto huo ulizuka ndani ya chumba hicho na kuteketeza kila kitu pamoja na kifo cha kichanga hicho kilichokuwa na siku 25 ambaye jina lake ni Zainab Abdala.
Moto huo ulizimwa kwa juhudi za wananchi wa eneo
Katika tukio jingine, Kamanda wa Polisi MKoa wa Kinondoni, Elias Kalinga alisema kuwa, mtoto David Jeras (7) alikufa maji baada ya kutumbukia katika mtu Mbezi.
Kalinga alieleza kuwa, mtoto huyo ambaye ni mwanafunzi wa Darasa la
Mahiti ya mtoto huyo iliopolewa na wananchi na imehifadhiwa katika Hospitali ya Mwananyamala kwa uchunguzi zaidi.
No comments :
Post a Comment
here u,re comments/acha ujumbe wako hapa