Sunday, May 9, 2010

 

 

 

JUKWAA LA WAHARIRI LAJIPANGA NA UCHAGUZI MKUU-2010

 

  Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA, A.Nkya( kulia alipokuwa amekabidhiwa tuzo

 

Na Mwanablog wetu

 

JUKWAA la Wahariri limekemea vikali  baadhi ya Wanasiasa ambao wanatumia vibaya  vyombo vya  Habari kutoa Habari za uongo kwa lengo la kuwachafua wengine, ni hila na zengwe za kiongozi hasiyefaa.

 

Hayo yalibainishwa katika taarifa iliyotolewa mapema leo katika vyombo vya  Habari na kusainiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa  Chama Cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA), Ananielea Nkya, kufuatia mkutano wa Wahariri waandamizi zaidi 60 walioudhuria mkutano  huo wa mikakati ya kufanikisha uchaguzi Mkuu na kuzuia mimba  mashuleni.

 

Taarifa hiyo, ilisema kuwa, jukwaa hilo litasimamia kidete kuona  nchi inajiandaa kwa uchaguzi mkuu wa mwezi Oktoba mwaka huu na kufanya vyombo vya habari kutekeleza wajibu wa kuwezesha uchaguzi  kuwa wa huru na amani.

 

"Vyombo vya Habari wanatambua nguvu ya kuhakikisha Umma na umuhimu wa Habari kuwezesha uchaguzi kuwa wa huru na wa haki, hii ni pamoja na kuepuka  kuandika na kutangaza habari zinazochochea chuki  kwa misingi ya ukabila,imani ya dini na jinsia"  ilisema katika taarifa hiyo.

 

Wahariri hao pia, walisema wanaweza kulisaidia Taifa kuepuka watu waovu kupata  uongozi kwa kuandika Habari zitakazoweka bayana vigezo ambavyo mtu yoyote anayetaka kugombea uongozi atalazimika kuwa navyo.

 

Aidha, jukwaa hilo, limewapa changamoto wagombea na vyama vyao kuanza kujenga tafsiri pana ya ushindi ili uchaguzi uwe kukuwa na manufaa makubwa kwa Taifa. Uchaguzi unaofanyika katika misingi hiyo ya Haki,uhuru na amani, inawatayarisha wanaoshindwa kupokea matokeo kwa heshima na hivyo kuepusha ghasia baada ya matokeo kutangazwa.

 

Hivyo, ni muhimu wanasiasa kutambua kuwa, asiyekubali kushindwa si mshindani

 

"Wamesema si vema ushindi uikahesabiwa kuwa idadi ya kura pekee, bali pia ni kwa jinsi gani uchaguzi utakuwa umefanyika kwa misingi ya Haki,Uhuru na bila rushwa ilikuimalisha amani, utulivu na demokrasia nchini".

 

 

Kuhusu suala la mimba mashuleni, jukwaa hilo  limeshauri Serikali  kuhakikisha inatengeneza mtaala mpya wa elimu  utakao toa elimu kumwezesha mwanafunzi kujitambua.

 

"Mtaala wa sasa hauna uwezo wa kumsaidia  mtoto kujitambua na kutoa maamuzi sahihi juu ya maisha yake,hivyo ni bora Serikali kuliona hilo".

 

Huku wakishauri  mashirika yasiyoya kiserikali kushirikiana na vyombo vya Habari kuanzisha mjadala wa kitaifa utakao wezsesha kutambua haki zao  na kujikinga vishawishi vya kupelekea kupata mimba mashuleni.

 

Aidha, maadhimio mengine walifikia wahariri hao, ni kuhakikisha wanaimarisha jukwaa lao ili liweze kuwa chimbuko la kusaidia wahariri kuimalisha taaluma na maslahi yao pamoja na wanahabari.

 

 

 

 

 

 

 


No comments:

Post a Comment

here u,re comments/acha ujumbe wako hapa