JKT yatangaza nafasi za kazi
Na Mwanablog wetu
Wakuu wa Jeshi la Kujenga Taifa JKT
JESHI la Kujenga Tifa (JKT) limetangaza nafasi za kazi kwa Vijana wa kujitolea kujiunga kwa mkataba wa miaka miwili.
Katika taarifa ya tangazo lililotolewa kwenye vyombo vya Habari hivi karibuni na Ofisi ya Habari makao makuu ya jeshi hilo Mlalakuwa jijini Dar es Salaam, zilielewza kuwa jeshi ilo litaandikisha Vijana wa kujitolea kwa hiari kutoka Vijijini na Mijini kwa mkataba wa miaka miwili kulitumikia Taifa.
Zoezi hilo, ambalo linazia Mei mwaka huu, litakuwa ni la nchi nzima huku mshari na sifa za kujiunga kwa vijan hao ni lazima awe Mtanzania umri kuanzia miaka 18 hadi 23, elimu ya kuanzia darasa la Saba na kuendelea, asiwe ameoa au kuolewa na wala asiwe na mtoto pamoja na kutokuwa na historia ya uhalifu wa kutumia silaha ama kushitakiwa kwa makosa ya jinai.
Kwa vijana waliokwisha pitia mafunzo ama kujiunga na majeshi ya JWTZ, JKT, Polisi, Magereza, KKM, JKU na Chuo cha mafunzo hawaruhusiwi kutuma maombi hayo.Pia awe tayari kufuata sheria zote za Kijeshi zitakazo kuwa juu yake pamoja na maagizo mbalimbali yatakayokuwa yakitolewa mara kwa mara na viongozi wake.
Pia awe tayari kulitumikia taifa kwa kushiriki kikamilifu katika shughuli mbalimbali za ndani ya JKT kwa kipindi cha miaka miwili na awe tayari kurudi nyumbani baada ya kumaliza mkataba.
Aidha, kila kijana aliye na sifa hizo na anapenda kujiunga na jeshi hilo, wanatakiwa kutuma maombi yao kupitia Serikali za Vijiji na Mitaa wanayoishi huku usaili na michujo itafanywa na kamati za Ulinzi na Usalama za Mikoa.
…
No comments:
Post a Comment
here u,re comments/acha ujumbe wako hapa