| Watu 19 wauwawa katika machafuko ya Thailand ![]() | ||||
| Waandamanaji waliovalia shati nyekundu katika mji mkuu wa Thailand, Bangkok, wamesema wataendelea kushinikiza kufanyika kwa uchaguzi wa mapema, siku moja baada ya kutokea kwa mapambano makali ya kisiasa kuwahi kutokea nchini humo katika kipindi cha miaka ishirini sasa. Kwa uchache watu kumi na tisa, wakiwemo raia na wanajeshi wameuwawa katika mapambano hayo ya siku ya Jumamosi. Wanajeshi wa serikali walitumia risasi za mpira dhidi ya waandamanaji, na kisha kuondoka katika maeneo ya mapambano. Waandamanaji wameonekana wakipanda magari ya kijeshi yaliyotelekezwa mjini Bangkok. Japan imeonyesha wasiwasi kuhusu kifo cha moja wa raia wake, ambaye alikuwa mpiga picha wa shirika la habari la Reuters. | ||||

No comments :
Post a Comment
here u,re comments/acha ujumbe wako hapa