WALIOMUUA DEREVA TEKSI WAKAMATWA MORO
andengenye
POLISI mkoani hapa imefanikiwa kuwakamata watu watatu kati ya watu kadhaa waliohusika mauaji ya dereva teksi Ibrahimu Mohamed (31) mkazi wa Mazimbu Manispaa ya Morogoro kisha kupora gari
Watuhumiwa hao ni Hamad Kisonga (26) mkazi wa Chang'ombr Dodoma, Maximilian Mushi (62) na Frenk Shirima (31) wakazi wa Msamvu Manispaa ya Morogoro ambapo walikamatwa Aprili 5 mwaka huu majira ya jioni kwenye nyumba ya wageni ya White Rose iliyopo maeneo ya Msamvu Mjini hapa.
Jitihada za kufanikisha kuwakamata watuhumiwa hao zilitokana na taarifa kutoka kwa raia wema ambao waliwatilia mashaka watuhumiwa hao pamoja na wengine ambao walikimbia mara baada ya polisi kufika katika nyumba hiyo na hivyo polisi kufanikiwa kuwatia mbaloni watuhumiwa hao watatu.
Kati ya watuhumiwa hao waliokamatwa ni pamoja na Mmiliki wa nyumba hiyo Maximilian Mushi ambaye pia ni mzee wa kanisa la KKKT usharika wa mji mpya na baada ya polisi kufanya upekuzi katika nyumba hiyo pia yalikutwa magari matatu ambayo ni Toyota Pick up, Hiece na Isuzu Trooper iliyokuwa na namba za serikali kwenye kioo cha dirisha iliyosomeka kama SU 26422 hata hivyo magari yote yalitolewa namba za mbele na nyumma hali iliyoleta mashaka kwa polisi
Mmiliki wa nyumba hiyo alikamatwa na kushikiliwa baada ya polisi kumtilia mashaka katika kuhusika na tukio hilo pamoja na matukio mengine hasa kwa kuzingatia kuwa watuhumiwa hao walifika katika nyumba hiyo siku tano kabla ya kufanay mauaji ambapo siku ya tukio walirudi usiku wa manane huku wakiwa na gari lisilo na namba na lililolowa damu na yeye kuruhusu gari hilo kuingia ndani na kukaa kwa siku nne bila ya kutoa taarifa.
Polisi baada ya kufanya upekuza zaidi kilikutwa kiatu kimoja cha marehemu, matambara yaliyotumika kumziba mdomo, mkanda wa kijeshi, sitikava za gari
Akihojiwa na polisi mtuhumiwa Kisonga alidai kuwa yeye na wenzake akiwemo mwanamke mmoja ambaye alikuwa kama chambo kwa kumkodi marehemu walitokea Dodoma na walitumwa na mwanamke waliyemtaja kwa jina moja la Maimatha wa mjini Dodoma ambaye aliwataka wamuue dereva teksi huyo kwa malipo ya Sh 5 milioni lakini wao waliingia tamaa ya kuchukua gari hilo ili kuongeza kipato.
Aidha mtuhumiwa huyo pia alimtaja mwenyeji wao mjini hapa ambaye alishirikiana nao kufanya njama za kumuua dereva huyo kuwa ni Ramadhani Kasanga mkazi wa Kiwanja cha Ndege ambaye pia polisi wanamtafuta baada ya kutoroka.
Kufuatia tukio hilo Kaimu Mwenyekiti wa mtaa wa magodoro kata ya Mwembesongo Thomas Somba alisema kuwa tukio hilo ni la mara ya kwanza kutokea katika nyumba hiyo ya kulala wageni lakini tayari kulishakuwa na mashaka na wageni wanaofika katika nyumba hiyo kutokana na mazingira iliyopo, jengo la nyumba
Pia aliwapongeza raia wema waliotoa taarifa za mashaka juu ya watuhumiwa hao pamoja na polisi kufanikisha kukamata baadhi ya watuhumiwa na kuongeza kuwa serikali ya mtaa huo ipo tayari kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi katika kuwafichua waharifu hasa wa ujambazi ambao wameonekana kutumia eneo
Waandishi wa habari hizi walishuhudia umati wa watu wakiwemo madereva teksi wa mjini hapa ambao walikuwa wakishuhudia watuhumiwa hao wakikamatwa huku watu wananchi wengine wenye hasira kali wakiwaomba polisi wawaruhusu japo kidogo tu kutoa kipigo ili wamalize hasira zao.
Kamanda wa Polisi mkoani hapa Thobias Andengenye alithibitisha kukamatwa kwa watuhumiwa hao wa mauaji na ujambazi na kwam,ba uchunguzi zaidi unaendelea ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kuwa wote waliohusika katika tukio hilo wanakamatwa na kufikishwa mahakamani haraka.
No comments :
Post a Comment
here u,re comments/acha ujumbe wako hapa