VIONGOZI WA DINI WAONYWA: WATAKIWA KUKATAA KUTUMIKA KISIASA

MKUU wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Askofu Dk. Alex Malasusa amewashauri viongozi wenzake wa dini kutotumia nafasi zao kuwapigia debe wanasiasa ili wachaguliwe na waumini wao katika uchaguzi mkuu utakaofanyika mwezi Oktoba mwaka huu.
Dk. Malasusa aliyasema hayo jana katika salamu zake za sikukuu ya Pasaka katika Ibada ya Kitaifa iliyofanyika katika Kanisa Kuu la Azania Front jijini Dar es Salaam.
Alisema kwa sababu mwaka huu ni wa uchaguzi baadhi ya viongozi wa dini watatumiwa na wanasiasa ili wawahubirie wananchi wawachague kama ilivyo kwa mataifa mengine ambayo yametumia maandiko ya neno la Mungu ili kuwanadi baadhi ya viongozi.
"Uchaguzi huu si wa kwanza kwa taifa letu, lakini mimi mpaka sasa nimeona hofu hasa ya mwamko wa wale wanaotaka kuchaguliwa jinsi wanavyoonesha msukumo wa ajabu na wanatafuta watu wawape fedha ili wachaguliwe… wanasiasa wasifikiri mimi ninaweza kuwahubiria watu wawachague," alisema.
Mkuu huyo wa Kanisa alisema inabidi viongozi wa dini waamke na kuwahubiria waumini wao watambue watu wenye uzalendo na wajiulize hao wanaotaka kuchaguliwa kwa fedha ili wapate uongozi ni kwa manufaa yao au ni kwa manufaa ya taifa.
Askofu huyo alisema kwa sasa Mataifa ya Afrika yana sifa mbaya na yanatambulika kwamba baada ya uchaguzi ni vita vya ndani na ni kutokana na hao wenye uchu wa madaraka ambao hugawa fedha ili waingie madarakani na baadaye kusababisha vita vinavyopelekea vifo vya wananchi wasio na hatia.
"Ni aibu sana kwa mataifa ya Afrika kupata sifa ya malumbano ya uchaguzi… Taifa letu linaendelea kuwa maskini mwaka hadi mwaka kutokana na kuchagua viongozi wasiofaa. Kwa sasa tuseme haiwezekani tena taifa likaendelea kuwa maskini tutafute watu wa kweli na watakaotutoa katika umaskini na wenye uzalendo na nchi yao," alisema.
Alisema kama rushwa itaendelea kutolewa ili wapatikane viongozi, taifa litakufa maana ni chukizo kwa Mungu na yatatokea machafuko kama yalivyotokea kwa mataifa ya jirani na kuwataka waumini kuwa chumvi ya ulimwengu kwa kukataa rushwa ili yasije yakajitokeza mapigano.
"Ikiwa Taifa hili linaongozwa kwa kunuka rushwa sisi Wakristo tukatae na hili litawezekana kama neno la Mungu litakuwa ndani yetu maana alituambia sisi ni chumvi ya dunia na itakapoharibika hatutafaa tena." alisema.
Alisema kama rushwa hii ikiendelea tunapoelekea tajiri na maskini watakuwa na tofauti kubwa sana ingawa Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere alilipinga hili.
"Kwa kweli tusipoangalia kwa umakini siku zinavyozidi kwenda mbele kutakuwa na tabaka kubwa na wapo masikini wanaendelea kuwa masikini kila kukicha huku matajiri nao wakiendelea kuwa matajiri kila panapokucha na hii inatokana na upofu unaosababishwa na rushwa" alisema.
Pia Dk. Malasusa alivitaka vyombo vilivyowekwa kutoa haki vitoe haki hiyo kwa wakati na kwa haraka hasa kwa wale waliotuhumiwa kwa ubadhirifu wa mali za umma kesi zao zisikilizwe kwa haraka na haki itendeke.
Katika hatua nyingine alisema kuwa wanawake ni jeshi kubwa kama maandiko yanavyoeleza na kwamba wanaweza kama wakiwezeshwa hivyo aliwataka kujiamini na wawe wajasiri bila kuyumbishwa ili wajitose katika uchaguzi.
Akitoa salamu kwa niaba ya waumini, Mkurugenzi wa TAMWA, Ananilea Nkya aliwataka wanawake kuendeleza ujasiri wao na kutokukubali kutumiwa na wajanja au shetani. Ibada hiyo ya sikukuu ya Pasaka ikiwa ni kumbukumbu ya Kufufuka kwa Yesu Kristo ilihudhuriwa na waumini pamoja na viongozi mbalimbali wa dini, kitaifa, vyama vya siasa na watu mashuhuri.

No comments :
Post a Comment
here u,re comments/acha ujumbe wako hapa