Translate in your language

Wednesday, April 7, 2010


SPLM kususia uchaguzi wa ubunge Sudan
 


Mzozo wa uchaguzi mkuu nchini Sudan unaendelea kukithiri huku chama cha Sudan's Liberation Movemnet- SPLM kikitangaza kususia uchaguzi katika maeneo mengi ya kaskazini mwa nchi hiyo.

SPLM kitasusia uchaguzi wa maeneo bunge na majimbo, katika majimbo kumi kati ya majimbo 15 yaliyoko kaskazini mwa nchi.


Hata hivyo chama hicho kitaendelea kushiriki uchaguzi katika eneo la kusini ambako kina umaarufu mkubwa.

Wiki jana SPLM ilitangaza kujiondoa kwenye mchuano wa urais, msimamo uliochukuliwa na vyama vingine vya upinzani.


Katibu Mkuu wa SPLM, Pagan Amum amesema wanasusia uchaguzi kuonyesha kutoridhika kwao na hali ya usalama huko Darfur na hofu ya kuwepo na wizi wa kura.


Huu ndiyo uchaguzi wa kwanza kuvihusisha vyama vingi vya kisiasa tangu mwaka wa 1986.


No comments :

Post a Comment

here u,re comments/acha ujumbe wako hapa

Kijiweni (nipe 5)