RAIS KIKWETE KUONGOZA SIKU YA MALALIA DUNIANI!!
Na Mwanablog wetu
Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete anatalajiwa kuwa mgenji rasmi siku ya maadhimisho ya ugonjwa Malaria yatakayofanyika Aprili 25 katika viwanja vya Mnazi Mmoja, ambapo kwa
Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa leo jijini Dar es Salaam na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii,Profesa David Mwakyusa (MB) alisema hiyo ni fursa ya kipekee kwa Tanzania kuadhimisha siku hiyo ya Malaria Dunia, iliyokuwa na kauli mbiu ya "TUSHIRIKIANE KUTOKOMEZA MALARIA".
Mwakyusa alisema kuwa, kwa Tanzania kuadhimisha siku hiyo ni fahari ya pekee, huku macho yote ya wataalamu wa Mambo Duniani wakiwemo Wanasayansi,wanaharakati,wanasiasa,washiriki wa maendeleo na wanahabari na wapambanaji wa ugonjwa huo watayaelekeza siku hiyo ambayo ni ya Kihistoria kwa Watanzania.
"Hii ni kutokana na jitihada zetu za kupambana na ugonjwa huu wa Malaria, bila shaka zimeonekana, nijukumu letu sote sasa kuitunza heshima hii kwa kuongeza kasi katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa Malaria" alisem Mwakyusa.
Siku ya Malaria ufanyika kila terehe 25 ya kila mwezi wa Aprili, ambapo kihistoria siku ya Malaria ilianza kuadhimishwa Aprili 25 mwaka 2000 baada wa nchi kukutana Abuja Nageria na kuamua kwa pamoja kuadhimisha kila ifikapo tarehe hiyo ilikuokoa madhara kwa jamii pamoja na kukumbuka jamii iliyokumbwa na ugonjwa huo ambapo ilijulikana kama "Siku ya Malaria Afrika".
Hata hivyo kuanzia mwaka 2008, ilibadilika na kuwa, siku ya Malaria Duniani, baada ya maafikiano ya mkutano wa Geneva Uswis katika mkutano wa 60 wa Afya Duniani mwaka 2007.
Mikakati ya kila nchi ni kupambana na ugonjwa huo kwa nguvu zote na kuhakikisha wanautokomeza ilikupunguza vifo kwa wananchi Duniani. Kwa Tanzania, Mwakyusa aliwataka watanzania kupigana kwa hali na mali ilikuhakikisha wanaushinda ugonjwa huo ambao ni chanzo kikibwa cha umasikini,Afya duniani na vifo vya wananchi wengi hususani watoto na walio na umri wa miaka mitano na akina mama wajawazito.
Hivyo kwa kuona umuhimu wa kupambana na ugonjwa huo, Tanzania katika kuhakikisha inapiga hatua uimeweza kufanya mambo mbalimbali kwa wanachi dhidii ya ugonjwa huo, Mwakyusa aliytaja mambo hayo kuwa ni pamoja na : Tanzania kuanzisha kampeni maalum ya Zinduka iliyozinduliwa na Rais Kikwete ambaye ni Mwenyekiti wa mwanzirishi wa wa Umoja wa Viongozi wa Afrika wa kupambana na Malaria, ALMA.
Kushiriki katika chanzo ya kutokomeza Malaria, Taasisi ya Afya ya IFAKARA imeweza kujulikana ulimwenguni kutokana na tafiti zake za ugonjwa huo, visiwa vya Zanzibari vimeweza kukabiliana na ugonjwa huo mpaka kuushinda na kuwa mfano wa kuigwa duniani kote, kutoa huduma za Afya kwa bei nafuu, kugawa dawa za ugonjwa huo zikiwemo za ALU na mseto, kugawa vyandarua vya kudummu ambavyo vinadawa maalum ya kufukuza mbu na mengine mengi.
Mwakyusa alisema kuwa, mpaka sasa
Huku idadi ya wagonjwa wanaokufa ni takribani 20,000 kila mwaka ambao kati
No comments:
Post a Comment
here u,re comments/acha ujumbe wako hapa