Translate in your language

Friday, April 16, 2010

Mdahalo wa kihistoria wafanyika Uingereza
Kwa mara ya kwanza katika historia ya siasa za Uingereza, viongozi 
wa vyama vikuu vitatu vya kisiasa nchini humo wameshiriki mdahalo
wa uchaguzi wa nafasi ya waziri mkuu.
Mdahalo huo ulionyeshwa moja kwa moja kupitia televisheni.
Waziri mkuu Gordon Brown, na wapinzani wake, David Cameron wa chama
cha Conservative na Nick Clegg wa Liberal Democrats, walijibu maswali
mbalimbali yaliyoulizwa na watu walioalikwa kwenye mdahalo huo.
Maswali hayo yalihusu mada mbalimbali ikiwa ni pamoja na uhamiaji na 
namna ya kutatua suala la nakisi ya bajeti ya Uingereza.
Midahalo mingine miwili ya televisheni ikilenga masuala ya nje na uchumi wa
Uingereza, imeandaliwa kufanyika kabla ya siku ya uchaguzi , tarehe sita Mei 
mwaka huu.
Maoni ya haraka baada ya mdahalo huo yamempa ushindi bwana Clegg
ambaye chama chake kinaweza kuleta uwiano katika uongozi wa nchi hiyo
baada ya uchaguzi

No comments :

Post a Comment

here u,re comments/acha ujumbe wako hapa

Kijiweni (nipe 5)