| Goodluck hajaonana na Rais Umaru Yar' Adua ![]() | ||||
| Kaimu rais wa Nigeria Goodluck Jonathan,anasema hajawasiliana na rais Umaru Yar'Adua kwa miezi mitano. Bwana Yar'Adua hajaonekana hadharani tangu aliporejea kutoka nchini Saudi Arabia kwa matibabu mwezi Februari.
Akiongea na BBC, bwana Jonathan hakuelezea chochote kuhusu afya ya rais Yar' Adua ingawa alisema amezungumza na mkewe pamoja na wasaidizi wake.
Aidha alizungumzia ghasia zilizokumba jimbo la Jos akisema zilichochewa kikabila wala sio kidini. | ||||

No comments :
Post a Comment
here u,re comments/acha ujumbe wako hapa