| Ban Ki Moon ataka viongozi Guinea Bissau kuwa na Amani ![]() | ||||
| Katibu mkuu wa umoja wa mataifa, Ban Ki-moon, ametoa wito kwa viongozi wa kijeshi na kisiasa nchini Guinea Bissau kutatua tofauti zao kwa njia ya amani. Wito huo umetolewa baada ya wanajeshi walioasi, kumtia mbaroni waziri mkuu wa nchi hiyo na mkuu wa majeshi aliyengolewa madarakani. Rais wa nchi hiyo Malam Bacai Sanha amefanya mazungumzo na wawakilishi wa wanajeshi hao waasi na kusema hali ya utulivu imerejea. Awali naibu mkuu wa majeshi wa nchi hiyo generali Antonia Njai alisema wanajeshi wote nchini humo wako chini ya amri yake. Tangu Guinea Bissau ilipopata uhuru mwaka wa 1974 kumekuwepo na mapinduzi kadhaa ya kijeshi nchini humo. | ||||

No comments :
Post a Comment
here u,re comments/acha ujumbe wako hapa