Thursday, August 18, 2016

MLIPUKO WA UGONWA WA HOMA INI (HEPATITIS B)

Waziri wa afya Ummy Mwalimu kupitia gazeti la habari la tarehe 9/8/016 amesema homa ya ini (Hepatitis B) kwa sasa ni tishio kushinda ukimwi.

Shirika la afya duniani (WHO) leo kupitia shirika la utangazaji (BBC) limekiri kuwepo kwa mlipuko mkubwa wa ugonjwa huo ktk nchi ya Angola na Jamuhuri ya Kongo. Mlipuko huo ni mkubwa kuwahi kutokea zaidi ya miaka 30 iliyopita,ambapo watu zaidi ya nusu milioni wameambukizwa na tayari watu 400 wameshafariki na inahofiwa kusambaa ktk nchi nyingine.

Mlipuko huu umesababisha uhaba mkubwa wa chanjo, na kulazimika kupunguza dozi ya chanjo na kwa sasa dozi ya mtu mmoja inatumika kwa watu watano,ili kuwapa kinga walau ya mwaka mmoja badala ya miaka kumi.

NB.ifahamike kuwa,ugonjwa huu hauna tiba na kinga ni bora sio tu kuliko tiba,bali hamna tiba.

Kwa dsm chanjo inapatikana mnazi mmoja hospital,bandari,regency,da two kisutu n.k.gharama ya kipimo ni 10000/=na chanjo ni 31000/= na unatakiwa kupata chanjo 3 ndani ya miezi 6.

Nashauri kila mtu achanje familia yake.

No comments:

Post a Comment

here u,re comments/acha ujumbe wako hapa