Tuesday, March 1, 2016

Dk.Kigwangalla aagiza kusimamishwa kazi kwa Wauguzi sita wa Hospitali ya Temeke kwa kuomba rushwa

Wauguzi sita wa wodi ya akinamama Wajawazito wa hospitali ya rufaa ya Temeke,wamesimamishwa kazi kwa kukiuka maadili ya taaluma yao wakati wa kuwahudumia akina mama wanaofika kujifungua kwenye hospitali hiyo.
Hatua hiyo imefikiwa kwenye ziara iliyofanywa hospitalini hapo na Naibu waziri, wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,wazee na Watoto, Mh. Dkt. Hamisi Kigwangwalla alipofanya ziara ya kawaida kuangalia utendaji wa kazi aliyofaya mapema leo Machi Mosi. (Machi 1.2016).
Tukio hilo la aina yake, ni mara baada ya Dk. Kigwangalla kufika Hospitalini hapo na kuangalia huduma zinavyotolewa pamoja na kusikiliza wagonjwa, ghafla baadhi ya wagonjwa walipobaini uwepo wa Naibu Waziri huyo ndipo walipomfuata na kutoa maoni na kero zao ikiwemo suala hilo la kudaiwa pesa za matibabu na dawa licha ya kuwa wana kadi za bima za matibabu.
Hata hivyo baada ya Dk. Kigwangalla kuhoji juu ya malalamiko yao, ndugu wa wagonjwa hao walimweleza kuwa, licha ya kuwa na Bima ya Afya, mgonjwa wao ambaye alikuwa mjamzito Wauguzi walimtaka atoe pesa ili kulipia vifaa huku wakikataa kwa kutotumika kwa kadi ya matibabu hali ambayo ni kinyume na utaratibu.
Aidha,wauguzi hao wanatakiwa kifikishwa kwenye baraza la wauguzi na wakunga kwa kukosa uadilifu.
Waliosimamishwa kazi ni pamoja na Bi Beatrice Temba, Marian Mohamed, khadija Salum, Elizabeth Mwilawa, Agnes Mwapashe na Merion saidi.

Hatahivyo, Dk. Kigwangalla ametoa siku 30 kwa Manispaa hiyo ya Temeke kukamilisha chumba cha upasuaji cha akina mama Wajawazito. Pia ameagiza Vyumba viwili vya upasuaji kufanyiwa ukarabati mkubwa na kuwa katika ubora unaotakiwa ndani ya miezi sita.
Aidha, ametoa miezi mitatu kwa chumba cha watoto wachanga kwa kuongeza vitanda 25 hadi 30 kutoka vitanda 9 vya awali ili kuepusha magonjwa ya kuambukiza ambapo kwa sasa wodi hiyo ina vitanda tisa pekee huku wakiwa wanazalisha watoto zadi ya 30 kwa siku.
Dk.Kigwangalla ametoa wito kwa uongozi wa Hospitali hiyo kuhakikisha wanatekeleza yale yote aliyoagiza kwani pindi atakaporejea tena ni kuchukua hatua kwa watakaozembea.
Tazama MO tv, kuona video ya tukio hilo hapa:

Imeandaliwa na Andrew Chale, Modewjiblog/MO tv
dk hk yyyNaibu waziri, wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,wazee na Watoto, Mh. Dkt. Hamisi Kigwangwalla pamoja na Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo ya rufaa ya Temeke, Dkt.Amani Malima wakiwa katika moja ya maeneo ya Hospitali hiyo mapema leo
dk hk nmNaibu waziri, wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,wazee na Watoto, Mh. Dkt. Hamisi Kigwangwalla (katikati) akisikiliza kwa umakini maelezo ya Mganga Mfawidhi wa hospiyali hiyo, Dk. Malima.
dk kigwangalla gjNaibu Waziri Dk. Kigwangalla, Mganga Mfawidhi pamoja na ndugu wa mama Mjamzito aliyeombwa pesa za vifaa na wauguzi, wakielekea kumuonyesha Naibu Waziri mgonjwa huyo..
dk uiWakielekea wodi ya akina mama wajawazito..
dk hk jNdugu wa mgonjwa akitoa maelezo yake kwa kina (aliyenyoosha vidole juu) ambapo hata hivyo wauguzi waliofanya kitendo hicho hawakuwa tayari 'kutumbuliwa majipuu' ndipo Naibu Waziri alipoamua kuchukua hatua kwa wauguzi wote sita ambao walikuwapo zamu ambao pia walimshughulikia mama mjamzito huyo, wasimamishwe kazi mara moja pamoja na kuchukuliwa hatua za kisheria katika mamlaka husika.
Dk KigwangalNdugu wa kiume wa mgonjwa akitoa malalamiko yake hayo..
dk hk ggggNaibu Waziri wa Afya, Dk. Kigwangalla akiwa ndani ya chumba cha Mahabara cha Hospitali hiyo..
dk hkaUkaguzi ukiendelea..
dk hkNaibu Waziri wa Afya. Dk. Kigwangalla akiwa katika wodi ya akimama wajawazito wakati wa ziara hiyo ya kukagua utendaji kazi..
KigwaNaibu Waziri akiwasili katika Hospitali hiyo ya Temeke..
dk kigwangallahNaibu Waziri wa Afya Dk. Kigwangalla pamoja Mganga Mfawidhi, Dk. Malima wakisikiliza kwa makini malalamiko ya baadhi ya wagonjwa na ndugu wa wagonjwa (hawapo pichani)..
dk hkNaibu waziri, wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,wazee na Watoto, Mh. Dkt. Hamisi Kigwangwalla akitoa maelezo kwa uongozi wa Hospitali hiyo juu ya kuchukua hatua stahiki kwa wauguzi hao pamoja na kufanyia kazi maelekezo yote aliyoyaagiza. (Picha zote na Andrew Chale,Modewjiblog/MO tv)

No comments:

Post a Comment

here u,re comments/acha ujumbe wako hapa