Katika ziara hiyo, Dk. Kigwangalla alibaini mambo mbalimbali kutoenda sawa ikiwemo suala la utendaji mbovu ambapo alitoa agizo la kumtaka Mkurugenzi wa Shirika la Elimu Kibaha wanaosimamia Hospitali hiyo kutoa maelezo ndani ya masaa 24 kama anafaa kubaki ama lah!.
Aidha, Dk. Kigwangalla amebainisha kuwa, hali aliyoikuta katika chumba cha kuhifadhia maiti ni mbaya hivyo ili kuondoa matatizo amelazimika kuifunga kwa muda huo wa siku tatu ili kufanyia marekebisho kwa baadhi ya mambo ndani ya chumba hicho cha mochwari hospitalini hapo.
Awali vyombo vya habari vilitoa taarifa mbalimbali juu ya Mochwari hiyo ikiwemo badhi ya maiti kuhifadhiwa nje na kuhatarisha afya za wananchi.
Tazama MO tv, kuona tukio hilo hapa:
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla (katikati) akiwa na uongozi wa Hospitali hiyo akiwemo Mganga Mkuu wa Hospitali, Dk. Peter Datani (kulia) akitembelea katika hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Pwani-Tumbi wakati wa ziara hiyo mapema jana Machi 10.2016.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla akikagua Mochwari ya Hospitali ya Rufaa ya Tumbi
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla akikagua Mochwari hiyo. Ambapo hadi sasa licha ya matatizo inayoikabili mochwari hiyo haina umeme na vifaa muhimu ikiwemo kipima cha kupimia joto kuharibika.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla akiangalia kifaa maalum ndani ya Mochwari hiyo ambapo hata hivyo hakifanyi kazi.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla akitoa agizo hilo kwa uongozi wa Hospitali hiyo pamoja na viongozi wa Serikali juu ya kuifunga Mochwari hiyo kwa siku tatu hadi hapo itakapofanyia ukarabati mambo mbalimbali yanayoikabili Mochwari hiyo.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla alipowasilia kwenye Mochwari hiyo wakati wa ukaguzi huo katika Hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Pwani-Tumbi, mapema jana Machi 10.2016. (Picha zote na Andrew Chale, Modewjiblog-Kibaha,Pwani).
No comments:
Post a Comment
here u,re comments/acha ujumbe wako hapa