Mvumbuzi wa programu hii ya Kighana Herman Chinery-Hesse alitaka
kuchukua hatua dhidi ya matukio ya ujambazi wa kutumia silaha mjini
Accra. Ndivyo alivyokuja na programu hii ya "Hei Julor" au "Ewe mwizi"
kwa lugha ya wenyeji wa mji huo."Hei Julor" ni programu ya mfumo wa usalama inayotumiwa katika simu ambapo mtu anaweza kutuma ujumbe mtupu kutoka kwenye simu zaidi ya tano zilizosajiliwa katika eneo, pale makaazi ya mtu au biashara yanapovamiwa.
Hatua hii inasababisha kutumwa kikosi cha waokoaji kutoka kampuni binafsi ya ulinzi, na wakati huo huo watu wengine kumi wakiwemo majirani na marafiki wanapata ujumbe huo na wanaweza kufika haraka nyumbani kwa mhusika ili kumsaidia.
Huduma hii ya Hei Julor ilizinduliwa chini ya mwaka moja nyuma, wakati wa vuguvugu la mageuzi katika mataifa ya kiarabu na wakati ambapo maandamano ya vrugu yalikuwa yanafanyika nchini Uingereza.
kwa taarifa zaidi bonyeza hapa
No comments:
Post a Comment
here u,re comments/acha ujumbe wako hapa