Sunday, July 1, 2012

UZALENDO ??????

Madiwani 17 Chama cha Mapinduzi (CCM) wilayani Pangani, Tanga, wamesema hawana haja ya kuongezewa posho kutokana na kazi wanazofanya kisheria kuwa za kujitolea kama ilivyoainishwa kwenye Katiba.
Akizungumza kwa niaba ya wenzake , Seif Ali (Mapepo), alisema msimamo wao ni kutokubaliana na baadhi ya madiwani wenzao ambao wanadai waongezewe posho kama ilivyo kwa wabunge.
Alisema kukataa kwao kuongezwa posho hiyo kunatokana na ukweli kwamba udiwani si kazi ya ajira bali anatakiwa awe na shughuli zake binafsi za kumuingizia kipato.
“Unajua sisi madiwani tunatakiwa kuwa mfano katika jamii hivyo basi hakuna haja ya kudai tuongezewe posho kwa sababu fedha hazitoshi ukiangalia malipo wanayopewa wabunge bado haziwatoshi na wanadai waongezewe nyingine,” alisema Sefu.
Alisema hata kama madiwani hao wakiongezewa posho hiyo bado hazitoshi kutokana na hali ngumu inayosababishwa na mfumko wa bei nchini.

No comments:

Post a Comment

here u,re comments/acha ujumbe wako hapa