Monday, July 23, 2012

toka blog ya lady jay dee !!!! imenigusa nikaamua nami niiweke humu muione


IANGALIENI HII, SIJUI MTAITAFSIRI VIPI?? ILA MIMI IMENIFANYA NIJISKIE VIBAYA


Nilikuwa nimekaa nakula chakula, Ndani ya Restaurant moja hivi inaitwa PRIMI
wakaingia wazungu ambao kwa hisia nadhani waalikuwa ni familia moja, kama sio marafiki, katika kundi lao waliongozana na wasichana wawili wa kiafrika ambao wanaonekana dhahiri walikua sio wa mjini kutokana na matendo yao.

Kila mtu mle ndani alikuwa anageuka kuwaangalia kwa kuwashangaa, nikiwemo mimi manake sikutegemea, kitu cha namna hiyo kingeweza kutokea pale Restaurant

wasichana hao hawakukaa juu ya viti kama wateja wengine wote, bali waliomba mito ambayo waliiweka chini wakakalia.
walionekana kuwa busy kuchagua menu ambayo sina hakika sana kama walikuwa wanaweza hata kuisoma,
na walifanya hivyo bila kujali macho ya watu.

Ila wenzao waliokuja nao walikaa juu ya viti.
Nilielewa kuwa itakua ni mila na desturi zao ndizo ziliwapelekea kufanya hivyo, lakini pia nilijiskia vibaya kuwaona wamekaa chini wakati watu wengine wote wakiwa juu ya viti
Hizo ni hisia zangu, zinaweza kuwa sio sahihi pia

Cha kushangaza zaidi chakula kilipokuja mezani, wengine wote waliwekewa kwenye sahani za udongo....Lakini cha kwao kiliweka kwenye vyombo vya mbao mfano wa tray
Na style waliokua wanaitumia kula ni style mfano wa wanyama na sio binadamu....
Maana walipiga magoti wakainama wakaanza kula, kama vile wanavyokula wanyama....
GlaSS zao za Soda pia chini Sakafuni



Nilijiuliza tu, hao walioongozana nao walishindwa kuwaelekeza jinsi ya kula kama wanavyokula binadamu wengine????
Angalau tu wanapoongozana nao kwenye sehemu zenye macho ya watu wengi wenye tamaduni tofauti??

Hata ukienda nchi za kiarabu unajifunika, hata kama sio Muislam kufatisha mila zao....
Ingawaje mwisho wa siku kila mtu atadumisha mila na desturi zake
Nawasifu kwa mavazi, walipiga kitu cha kama Khanga hivi, Na pengine niwasifu pia kwa kulia chakula chini na kwa mikono manake hata sisi tunakula hivyo, ila sio kwa style waliotumia kula kama wanyama...Chakula chenyewe pia walishindwa kula hata robo ladha haikuwakolea

Niliomba kuwapiga hizo picha tu, sikuweza kuendelea zaidi ya hapo niliogopa

No comments:

Post a Comment

here u,re comments/acha ujumbe wako hapa