Friday, July 27, 2012

SIKU YA MASHUJAA TANZANIA

Rais Jakaya Kikwete (wa pili kushoto) akisalimiana na baadhi ya wazee waliopigana vita ya ukombozi dhidi ya wakoloni, wakati wa maadhimisho ya Siku ya Mashujaa, Dar es Salaam jana.









                                                                                  Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Bw. Pandu Ameir Kificho, akifurahia na Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Mstahiki, Dkt. Didas Masaburi (kushoto), mara baada ya Maadhimisho ya Siku ya Mashujaa, kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jana.














JK aongoza mamia Dar Siku ya Mashujaa

Na Goodluck Hongo (Majira)

RAIS Jakaya Kikwete, jana aliongoza mamia ya wakazi wa Dar es Salaam katika maadhimisho ya kumbukumbu ya Siku ya Mashujaa kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja.

Maadhimisho hayo hufanyika Julai 25 kila mwakakila mwaka ambapo watu mbalimbali walihudhuria wakiwemo mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao nchini.



Viongozi wa dini mbalimbali walitumia fursa hiyo kuwaombea mashujaa hao na Taifa kwa sala na dua.

Rais Kikwete ambaye ndiye alikuwa mgeni rasmi katika maadhimisho hayo, aliweka mkuki na ngao katika mnara wa kumbukumbu wakati Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Jenerali Davis Mwamunyange akiweka sime.

Wengine ni kiongozi wa mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao  nchini, Balozi Ibrahim Mukubi, ambaye aliweka shada la maua, Meya wa Jiji Dkt. Didas Masaburi, aliweka upinde na mshale ambapo kiongozi wa askari waliopigana vita ya pili ya Dunia Bw. Rashidi Bakari, aliweka shoka.

Katika viwanja hivyo, ilipigwa mizinga pamoja na gwaride ambalo liliandaliwa na vikosi vya ulinzi na usalama kwa ajili ya kutoa heshima kwa mashujaa waliokufa.

Kwa upande wake, Bw. Bakari aliiomba Serikali iwasaidie kupata haki zao kwani Serikali ya Uingereza imewatupa na kuwatelekeza mbali ya kuwaahidi kuwa itawalipa lakini hadi sasa iko kimya.

Naye Mzee Peter Achimpota, alisema vitani hakuna mshahara lakini Rais Kikwete aliwaahidi kuwapangia siku ya kuonana wazungumzie  suala hilo wakidai walipigana vita vya pili vya dunia mwaka 1939-1945 dhidi ya Ujerumani.

Viongozi wengine walioshiriki kumbukumbu hiyo ni pamoja na Makamu wa Rais Dkt. Mohamed Gharib Bilali, Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Alhaj Ali Hassan Mwinyi, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Ali Mohamed Shein.

Wengine ni Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Bw. Shamsi Vuai Nahodha na viongozi wa kijeshi kutoka China na Marekani.

No comments:

Post a Comment

here u,re comments/acha ujumbe wako hapa