Majira ya asubuhi siku ya jumatano meli ya mizigo Mv SAHARA inayofanya shughuli zake kati ya Dar Mafia na Zanzibar iliungua moto katika bandari ya Mafia.
Habari ambazo bado hazijathibitishwa inasemekana umetokana na hitilafu ya machine wakati wafanyakazi wa meli hiyo wakiwa katika zoezi la kupakua mafuta yaliyokuwa katika meli.
Eneo la kibini la meli likionekana kuungua kwa kasi, huku gari aina ya kijiko ikijaribu kutoa gari lililokuwa katika meli hiyo kupunguza maafa yanayoweza kutokea zaidi
Baada ya juhudi za wananchi na wafanyakazi wa meli hiyo kufanikiwa kuuzima moto huo, lakini changamoto ni kubwa, hakukuwa na vifaa maalum vya kuzimia moto huo ilikuwa ni kuchota maji ya bahari na kumwagia, sijui ingekuwaje pale kusingekuwepo na maji hayo kwa maana maji kupwa
No comments:
Post a Comment
here u,re comments/acha ujumbe wako hapa