Saturday, March 24, 2012

TUMEONEWA, Bomoa Bomoa Dar!!!!

moja ya familia wakiwa nje baada ya nyumba waliyokuwa
wakiishi kubomolewa katika zoezi hilo
FAMILILIA kadhaa zilizokuwa zikishi katika nyumba za Kampuni ya  Reli (TRL) za Mamlaka ya Usimamizi wa  Bandari Tanzania zilizoko katika eneo la Gerezani Kariakoo, jijini Dar es Salaam, zimesema kitendo cha kubomoa nyumba hizo ni cha kuvunja sheria za nchi.
Mapema saa 11.00Alfajiri  ya jana, Kampuni ya Udalalali ya Yono Action Mart ya jijini Dar es Salaam, ilianza kazi ya kubomoa zaidi ya nyumba 50  zinazokaliwa na familia 106.Mmoja wa waathirika wa bomoa bomoa hiyo, Ramadhani Ali alisema kitendo cha kubomolewa kwa nyumba zao ni cha unyanyasaji wanaofanyiwa na Serikali.
mtoto akiwa amelala nje baada ya kufuatia ubomoaji huo
Kwa mujibu wa Ali, familia hizo hazikupewa  muda wa kuondoa vitu vyao kutoka katika nyumba hizo.“Sheria wanatunga wenyewe na wanazitumia wakati  wanapoona kuwa wanachofanya kina manufaa kwao, tunaambiwa hukumu imetoka jana sisi tumepatiwa taarifa za kutakiwa kuhama saa moja jioni ni mda gani huo kw amtu kuweza kuhamisha vitu vyake”alihoji .
Naye Jubilent Mlaki ambaye ni mkazi wa eneo hilo alisema kilio cha cha muda murefu ni fidia iliyokuwa imetengwa kwa ajili ya familia zilizokuwa zikiishi katika nyumba hizo.
Alisema nyumba hizo waliuziwa na Serikali lakini na kwamba walipoamuriwa kuhama walielezwa kuwa watalipwa fidia ya kati ya Sh16 milioni na Sh18 milioni kiasi ambacho kilipingwa na wamiliki.
“Mimi jana (juzi) sikwenda mahakamani lakini waliokwenda walikuja na kuniambia kuwa hakimu aliyetoa hukumu alitutaka kuondoka katika eneo hili ili kupisha mradi Magari yaendayo kasi DART kwa ajili ya maendeleo ya nchi, lakini kwanini hatukupewa hata muda wa kuhamisha vitu vyetu alisema Mlaki.Alisema anachokifahamu, mahakama inapotoa hukumu inatoa pia utaratibu wa namna ya kuhamisha wahusika ikiwa ni pamoja na kupewa notsi.
wanafamilia wakiwa hawajui la kufanya
mwanamama akimalizia toa vitu vyake
Katika eneo hilo ulikuwa umeimarishwa na askari wa Kikosi cha Polisi wa Kutuliza Ghasia (FFU) kwa kushirikiana na polisi wa kawaida waliokuwa ma silaha mbalimbali.
Pia kulikuwa na magari yenye kumwaga maji ya kuwasha, tayari kwa kuwadhibiti watu ambao wangethubutu kufanya fujo.
Barabara za Mtaa wa Lindi na Msimbazi, zilifungwa ili kuruhusu kazi hiyo kufanyika kwa amani na utulivu.
Habari za awali zilisema watu wawili walipoteza fahamu baada ya kupewa taarifa kuhusu kuvunjwa kwa nyumba zao
Habari hizo zilisema watu hao walisaidiwa na wenzao kwa kupepelewa hadi walipopata fahamu na baadaye kuondolewa katika eneo hilo.
Wakati nyumba hizo zikiendelea kubomolewa polisi,  iliwakamata vijana kadhaa kwa madai kuwa waitaka  kufanya fujo.Mkurugenzi wa kamapuni ya Yono Auction Mart Scholastica Kevela alisema kazi hiyo imefanywa bila matatizo.“Kazi haikuwa ngumu sana ingawa tumekesha katika eneo katika hili kujiandaa na bomoa bomoa,wakazi wengi wa eneo hili wamejitahidi tangu jana usiku kuhamisha vitu vyao,”alisema Kevela.
wengine walionekana kunusuru baadhi ya vifaa ambavyo
wanaweza chukua kwa ajili ya ujenzi sehemu nyingine
Bomoa bomoa hiyo imefanyika siku moja baada ya  hukumu ya kesi iliyokuwa imefunguliwa na wakazi hao kupinga kuhamishwa katika nyumba hizo.



No comments:

Post a Comment

here u,re comments/acha ujumbe wako hapa