Tuesday, January 17, 2012

Moratti athibitisha kumtaka Tevez

ROME, Italia

RAIS wa Inter Milan, Massimi Moratti amethibitisha kuwa sasa wametuma ofa ya pauni milioni 25 kwa ajili ya mchezaji wa Manchester City, Carlos Tevez.



Inter ilisema wiki iliyopita hawawezi kutoa maoni kuhusu Tevez, hadi lifanyike pambano dhidi ya mahasimu wao AC Milan wikiendi iliyopita ambapo waliibuka na ushindi wa bao 1-0.

Nerazzurri baada ya kushinda mara moja kocha, Claudio Ranieri na klabu waliulizwa kuhusu mchezaji huyo kutoka Argentina.

kwa mujibu wa sky sports, Ranieri hakujiweka karibhu na suala hilo lakini Moratti, hakupoteza muda kuthibitisha kuwa wameandaa ofa ya zaidi ya pauni milioni 20.

"Hakuna siri katika soka," Moratti  aliiambia Controcampo.

"Ofa ni euro miliioni 25. Sasa ni juu ya City kama watakubalia au la."

Moratti pia alikiri kwamba si Inter pekee inayomfukuzia Tevez, pia imo PSG na kuna klabu za Uingereza.

Habari za Inter kutaka kutoa ofa zimekuja wiki moja baada ya AC Milan, kujitoa kwenye mazungumzo baada ya Alexandre Pato kukataa kuhamia Paris St Germain.

"Hadi wakati huu inaonekana kuwa hatumhitaji Tevez, lakini soka inatoa majibu tofauti kwa kutegemea siku.

"Nitaendelea kuwa na wachezaji wote waliopo kikosini kwa sasa, lakini bado kuna muda hadi kuisha kwa dirisha la uhamisho. Tutasubiri kuona."

No comments:

Post a Comment

here u,re comments/acha ujumbe wako hapa