Machozi apagawisha Bilz, Sheta ..
MWANAMUZKI nyota wa muziki wa Bongo Fleva, nchini Hussein Machozi usiku wa kuamkia Nov 21 aliweza kupagawisha mashabiki wapenda burudani kwa nyimbo mbalimbali ikiwemo nyimbo yake mpya ya 'Asante' ambayo ilipagawisha mashabiki ndani ya ukumbi wa Kimataifa Club Billicanas uliopo katikati ya jijini la Dar es Salaam. Katika shoo, iliyoanza usiku wa manane, Machozi aliweza kukonga nyoyo kwa nyimbo zake kadhaa ikiwemo ya 'Ajiri yako', 'Mzimu', 'Za mwizi 40, 'kafia gheto' pamoja na kibao hicho kipya cha 'Asante', ndani ya shoo hiyo , ambayo alipanda na madansa wake, waliweza k upagawisho vilivyo na kufanya shangwe za mara kwa mara kutoka kwa mashabiki waliofurika ukumbini hapo. Aidha, kwa mujibu wa Dj Ibra ndani ya ukumbi huo, wiki hiyo, Msanii mwingine wa Bongo freva, Nurdin Bilal 'Sheta' anatarajia kuzindua albam yake ambapo atasindikizwa na wasanii nyota mbalimbali nani ya ukumbi huo. Wasanii watakao msindikiza Sheta katika uzinduzi wake huo ni pamoja na Mwana FA 'Binamu' anayetamba na kibao cha 'Alahiti', Barnabas, Amini, Dully, Ay, na wasanii wengine wengi ili kunogesha zuzinduzi huo. Kwa sasa Shata ambaye ni Rais wa Da stamina, anatamba na vibao vya Unidai, sikudai aliiyoitengeneza kwa a Marcho Chalii na vibao vingne. Mwisho
Sekondari ya Tirav wababe bonanza la Tupambane Organization
SHULE ya Sekonari ya Tirav ya Jeti Lumo jijini Dar es Salaam, imefanikiwa kutwa ubingwa wa kombe la la Tupambane Organization lililoshirikisha shule za Sekondari Kata ya Yombo Vituka. Katika Bonanza hilo, ambalo lilikutanisha timu za sekondari za Lumo, Montefoty, Tirav na St.Moses, lililofanyika kwa siku mbili kwa lengo la kutoa elimu ya Ujana katika VVU na upimaji wa virusi, lilishuhudia mchezo mkali na wa aina yake wa fainali ya bonanza hilo lilifayika mwishoni mwa wiki kwa timu hiyo ya Tirav SS Fc ikiinyuka Lumo SS Fc kwa bao 6-1 na kutawazwa kwa washindi wapya na St.Moses SS Fc wakiibuka washindi wa tatu kwa kuwabwaga Monte foty SS Fc. Awali uhondo wa Bonanza hilo, ilishuhudia, Monte forty SS Fc ambao waliua vibonde katika mshindano hayo, walikubali kichapo kichapo cha bao mbili bila dhidi ya Lumo SS Fc, huku Tirav S.S FC wao wakifanikiwa kuwabamiza bao tatu kwa moja, St. Moses S.S Fc. Mabingwa hao Tirav SS Fc, ilikua na wachezaji nyota mbalimbali akiwemo kipa wake mahiri aliyekua katika mafunzo maalum ya Aitrlrising star,Denis Dionis 'Odo Nombo' ambaye alikua mwiba kwa kuokoa mashuti ya wapinzani wake,wengine ni Juma Kalufya aliyekua akichezea Azam Fc, Under 17 kwa sasa Simba SC Un 17, pamoja na Abdul Lugume anaye chezea Villa Squad Fc, Un 17. Mashindano ya kila mwaka, washindi walipata zawadi mbalimbali ikiwemo vifaa vya michezo, ambapo Mwenyekiti wa Tupambane waliodaa hilo, Claudio Mnari alipongeza viwango vilivyoonyeshwa na watopto hao huku akitaka changamoto zaidi kwa mwakani kuongeza timu ikiwemo kutokja nje ya kata hiyo. "Mwakani tunatarajia kuongeza timu hili kuleta changamoto na pia wadau tunaomba kujitokeza ili kupiga tafu katika michezo" alisema Mnari. Mwisho |
No comments:
Post a Comment
here u,re comments/acha ujumbe wako hapa