Alphonce Shaibu na Bertha Samwel (mwananchi) BEI ya vyakula na nguo kwenye soko la Kariakoo, Dar es Salaam imezidi kushika kasi kutokana na msimu wa sikukuu ya Eid el Fitri. Wafanyabiashara wa nguo, Johnson Tito na Susan Marco, walisema bei za nguo zimepanda kutokana na gharama za usafirishaji na kuporomoka kwa shilingi dhidi ya dola ya Marekani. Naye Halima Said alisema hivi sasa bei ya nguo ipo juu na kwamba, nguo ambazo walikuwa wakinunua Sh20,000 imefikia Sh30,000. Saidi alisema sikukuu ni wakati wa mavuno kwa wafanyabiashara.Mfanyabiashara wa nguo, Neema Sanga, alikiri kipindi hiki cha sikukuu kuwa mavuno kwao, ndiyo maana wanapandisha bei. Kwa upande wa vyakula, Ofisa Biashara na Takwimu, Nikanor Omollo, alisema bei za vyakula zinatofautiana kutokana na matumizi kipindi cha sikukuu, vyakula kama mihogo, nazi, magimbi, viazi vitamu na viungo vya pilau bei yake ipo juu.“Leo (jana) nimetembelea sokoni nimeona baadhi ya vyakula vimepanda wala siyo vyote,” alisema Omollo. Mfanyabiashara mwingine wa vyakula, Mussa Hussein, alisema bei za vyakula kwa ujumla zipo juu kutokana na gharama za usafirishaji na ununuzi kutoka mikoni. |
▼
No comments:
Post a Comment
here u,re comments/acha ujumbe wako hapa