Tuesday, August 16, 2011

KUNA WATU WANA SHIDA LAKINI HAWAONEKANI NA KUSAIDIWA

AMENIPA NDELWA:   Mlemavu anayejituma  Send to a friend

Amenipa Ndelwa
kwa niaba ya mwananchi (Tumaini Msowoya)“Nyanya, nyanya, nyaya! Dada karibu niungishe nyanya! Ni bei poa kabisa.”Ilikuwa sauti ya mwanamke, ikitokea nje ya disirisha la basi, nililokuwa nikisafiria kwenda kijiji cha Pawaga, Wilayani Iringa.

Sauti hiyo, ilinifanya nifungue dirisha ili nimuonemwanamke aliyekuwa akiita wateja kwa sauti ya juu, ambyo ilionyesha kuwa alihitaji, kuungishwa bishara yake ya nyanya ambazo alikuwa amezihifadhi katika ndoo, aliyokuwa amejitwisha kichwani.Hali ya mwanamke huyo ilinistua kidogo, alipopata mteja na kutakiwa kummiminia nyanya hizo katika mfuko wake wa ‘rambo’.

Mahangaiko yake katika kumuhudumia mteja huyo, yalinifanya nigundue kwamba hana viganja, ndio maana akawa akilazimika kutumia mdomo kwa shinda kutokana na shingo yake kutonyooka, kufuatia ulemavu alionao.


Nililazimika, kukatisha safari yangu, walau nizungumze na mwanamke huyo ambaye niliamini ni miongoni mwa wanawake wenye ulemavu, wasiopenda kubweteka wakisubiri kuletewa kila kitu nyumbani.“Karibu nyanya dada yangu, nauza bei  rahisi sana, nusu ndoo ni sh 3,500,” ndivyo alivyokuwa akinikaribisha, mwanamke huyo anyaitwa  Amenipa Ndelwa, mkazi wa kijiji cha Kiwele, kata ya Kiwele, mkoani Iringa.

Anasema, ulemavu wake haumfanyi ashindwe kujishughulisha kiuchumi na kwamba, biashara hiyo ya nyanya ndiyo huitegemea katika maisha yake, ya kila siku.Anasema amekuwa ikihudumia familia yake, kama wanawake wengine wasio na ulemavu na kwamba, anategemewa na wazazi wake, ambao wamezeeka.

Maisha yake
Ndelwa alizaliwa miaka 30, iliyopita katika kijiji cha Kiwele akiwa mzima. Miaka mitatu baadae aliangukia kwenye moto ambao ulikuwa umewashwa kwa ajili ya kukaushia tumbaku, hapo ndipo alipopata ulemavu.

“Nilitumbukia kwenye moto wa kukaushia tumbaku. Sikumbuki ilikuaje kwa sababu nilikuwa mdogo, ila wazazi wangu walinisimulia kwamba, niliponea chupuchupu baada ya kuungua mwili mzima, isipokuwa kichwa na miguu,” anasema Ndelwa.

Anasema, pamoja na ulemavu huo, muda wa kuanza shule ulipofika alianza na baada ya kumaliza hakuweza kuchaguliwa kuendelea na masomo ya sekondari, kutokana na uhaba wa shule kwa wakati huo.Anasema, tofauti na watu walio na viganja, yeye hulazimika kutumia mikono yote miwili kushikia vitu, ikiwemo kuandika, kupika na kazi nyingine za nyumbani.Anasema kutokana na hali hiyo, kaka yake aliamua kumpeleka kwenye chuo cha Usaliwa, ili akajifunze ufundi cherehani.

“Nilienda kujifunza ufundi kwa miaka minne, nilipomaliza masomo sikuweza kushona kwa sababu ya ulemavu wangu. Tatizo kubwa lilikuwa kwenye upande wa kukata vitambaa, hivyo nikaamua kuachana na kazi hiyo,” anasema.

Alianza bishara ya nyanya, ambazo alikuwa akinunua na kuuza kwa wasafiri wanaopita kijijini kwao, kutokana na kijiji hicho kuwa karibu na barabara inayoelekea Pawa, eneo maarufu kwa kilimo cha mpunga, mkoani Iringa.

Wakati akiendelea vyema na bishara yake, alibahatika kupata mchumba ambaye aliamini kuwa angekuwa mume wake lakini ya kumpa ujauzito, na kumkimbia akidai kuwa hawezi kuishi na mwanamke wenye ulemavu.Anasema hakukata tamaa, japo aliyumba kiuchumi. Aliilea mimba yake wakati akiwa bado chini ya wazazi wake, huku akiendelea na biashara yake ya nyanya inga wakati huo hakuweza kuifanya vizuri.

Mwaka 2004, alikutana na kijana mwingine, ambaye alimueleza wazi kuwa yupo tayari kuishi nae.“Nilikuwa na hofu, lakini baada ya kuwafuata wazazi wangu, na kukubali kulipa mahari nilikubali kuolewa. Huyu hakunikimbia na amekuwa msaada mkubwa kwangu, na tumeshapata watoto wawili,” anasema Amenipa na kuongeza:

“Watu wengi wanamuuliza mume wangu, ilikuaje akanioa wakati ni mlemavu. Swali hili huwa linaniumiza, japo huwa sijali kutokana na ukweli kwamba, mume huyu ananijali na kunithamini.”

Aabainisha: Ndiye anayenipelekea mzigo wa nyanya barabarani kila siku, kunisaidia kupika na kazi nyingine, ambazo nashindwa kuzifanya,” anasema.Mume wa Amenipa, Nasibu Ng’angali anasema alimuoa mwanamke huyo, kutokana na mapenzi ya dhati na kwamba, haoni tofauti  yoyote.

 “Mke wangu hawezi kutumia kisu hivyo huwa nakata mboga na kila kitu, lakini pia nabeba mizigo na kazi zote za kilimo, nazifanya mimi kwa sababu nampenda. Ulemavu wake sio sababu ya kumnyanyapaa,” anasema Ng’angali.

Mafanikio katika biashara
Anasema mafanikio ya familia yake yanategemea bishara ya nyanya. “Nimesaidia kukamilisha ujenzi wa nyumba yetu, watoto wanasoma, kuvaa na kula chakula kizuri kutokana na bishara hiyo,” anasema.

Anaongeza kuwa, tenga moja la nyanya amekuwa akilinunua kwa Sh6,000 na baada ya kuuza hupata Sh12,000 huku kukiwa na faida ya nusu ya fedha aliyotumia kununulia.Anasema kwa siku, amekuwa akifanikiwa kuuza tenga mbili, fedha ambayo kwa kijijini, imekuwa ikiwafanya waishi maisha maziri.

Unyanyapaa
Amenipa  anasema bado jamii inamtizamo finyu kuwa mlemavu ni mtu asiyeweza kufanya jambo lolote, ndio maana amekuwa akitengwa, kwa kutopelekwa shule wala kupatiwa , ajira kirahisi.Anasema, waathirika wakubwa wa unyanyapaa huo ni wanawake ambao hubeba mzigo mkuwa wa kulea mtoto mwenye ulemavu, au walemavu wanawake wenyewe kutelekezwa na ujauzito, kama ilivyowahi kumtokea.

Anasema kama hali ikiendelea kuwa kimya, azma ya kupambana na umaskini na unyanyasaji wa kijinsia haitafanikiwa, kwa kuwa kundi hilo litakuwa limesahauliwa japo linateseka.

No comments:

Post a Comment

here u,re comments/acha ujumbe wako hapa