Monday, July 11, 2011

breaking news








Watoa huduma ya kwanza kufanyiwa fujo ni haki?



Caption; ya RED CROSS SIMBA NA YANGA
waliosimama pamoja 3, Kamanda msaidizi, Feruzi Mpiri wakishahuriana jambo na Katibu wa Action team, Amina Mwalimu juu ya hatua ya kufanya baada ya fujo iliyosababisha mashabiki kurusha makopo na chupa za maji taka, katikati ni mjumbe wa kikosi, Hasan Yunusi na kulia, mwenye riboni mkononi, mjumbe na bloger team, Andrew Chale.

Mapema jana, wakati wa mchezo wa Simba na Yanga kwenye hatua ya mchezo wa fainali kulitokea mambo makuu mawili ambayo hata hivyo kwa namna mmoja ama nyingine yameweza kugusa hisia tofauti zilizo sababishwa na mashabiki wa timu zote mbili.
 Mambo hayo ni pamoja na kitendo cha mashabiki wa Simba, kufanya fujo kwa kushinikiza kutolewa kwa mpiga picha mkuu wa magazeti ya Tanzania Daima na Sayari, Joseph Senga, kwa kile kilichodaiwa kuvaa vazi la Yanga.."Mashabiki hao walipaza sauti huku wakirusha chupa za maji na viatu walishinikiza mwandishi huyo mkongwe na mpiga picha kuu aliyeanza kazi hiyo tangu miaka 60...kwa hali hiyo baada ya kutolewa, mashabiki wa Yanga ambao kwa hila na ukakasi wa unazi waliokuwa nao, waliamua kuwapigia kelele wataalamu wa mambo ya Huduma ya kwanza kwa wachezaji wa kikosi cha Maafa na Uokoaji (Action Team) Tanzania Red Cross, Mkoa wa Dar es Salaam,  kwa kile walichodai kuwa walivaa mavazi ya Simba Sc.

Kwa hali hiyo hali ilibadilika kwani waliwarushia maji na mikojo iliuyokuwa kwenye chupa, hali iliyoamuliwa kutoka ilikuepusha usalama wao...Sasa hali ndio hiyo je?  kama hali inakuwa hivi kwa kuwafanyia fujo huduma ya kwanza ambao wanafanya kazi hizo kwa kujitolea tena kwa kupewa tu tshilingi mia tano ama buku yaani ya nauli ..munatoa taswira gani kwa vikosi vya kijamii kama hivi? 


Waziri mwenye dhamana na chama cha soka munawajibu wa kutoa elimu kwa mashabiki na jamii kwa ujumla kuwa Red Cross kama Red Cross hakifungamani na chama chochote cha kisiasa wala upande wowote wa kimaslai ni Shirika la kujitolea kwa hali na mali kwa moyo mmoja na kazi zinazofanywa uwanjani ..ni miongoni tu kwani watoa huduma ya kwanza sawa na madaktari bingwa na hao munaowaheshimu au kuwakubali ila kwa majukumu wao wanavaa mavazi yaliyo na msalama mwekundu ilikuendana na mikataba ya Shirika la kibinadamu.

Kwa tukio hilo tunarahani kwa nguvu moja kwani hali ilikuwa mbaya uwanjani na kikosi hicho hicho walichokitupia mawe na chupa za mkojo baada ya kuombwa kurudi kilirudi kwa moyo mmoja na kiliendelea kufanya kazi lakini kikiwa kimekaa upande wa mashabiki wa Simba na baada ya dk 8 Mungu mkubwa mashabiki waliokuwa wakitupa chupa na kuzomea mashabiki wa Yanga   walizidiwa na kuanguka kitendo kilichowasababishia kupoteza fahamu na wanakikosi kiliweza kutoa huduma kwa moyo ule ule wa sheria za Msalaba Mwekundu bila upendeleo ..na hilo bila shaka walijisikia aibu sana lakini Wanakikosi hawajakata tamaa na wataendelea kutoa huduma ilikuokoa maisha ya watu. bila kuangalia rangi udini ama ukabila na chama.



No comments:

Post a Comment

here u,re comments/acha ujumbe wako hapa