Tuesday, May 17, 2011

Rais Miss UN kutua nchini

Na Andrew Chale
RAIS Miss Umoja wa Mataifa, Neville Wiliams, na ujumbe wa kamati ya dunia ya mashindano hayo unatarajia kutua nchini mwishoni mwa mwezi Juni katika ziara ya ukaguzi sambamba na kufanya mkutano na vyombo vya habari nchini.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na rais wa Miss Utalii Tanzania, Gideon Chipungahelo hadi sasa mkataba wa awali ulisainiwa na waandaaji hao wa Miss Umoja wa Mataifa na taratibu za kufanyika kwa shindano hilo nchini zinaendelea, ikiwemo kutoa taarifa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA).
Chipungahelo alisema kwa hatua hiyo rais huyo atatua nchini na kufanya ziara ya ukaguzi na baada ya hapo atakamilisha mazungumzo na waandishi wa habari juu ya majumulisho atakayoyaona.
“Mpaka sasa kamati yetu na yao tumeshakamailisha mchakato wa awali na ujio huo utakuwa na changamoto, watafanya mkutano huo wa kimataifa na waandishi wa habari,” alisema.
Alisema ujio huo ukiwa nchini utafanya mikutano na viongozi mbalimbali wa mamlaka za Serikali, makampuni binafsi na mashirika ya umma ambayo yanaweza kudhamini fainali hizo za dunia kwa hapa nchini.
Ziara hiyo itakagua vituo mbalimbali vya Televisheni nchini ili kupata kituo cha kitakachoshirikiana na vituo vya nje kurusha na kusambaza matangazo ya moja kwa moja ya fainali hizo kutoka Tanzania.
Tanzania kwa mara ya kwanza walikuwa wenyeji wa shindano la Dunia la urembo (Miss Tourism World 2006) lililofanyika katika ukumbi wa Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam.
Chipungahelo alisema Tanzania imepewa heshima kwa mara nyingine mwenyeji wa shindano lingine la dunia ambako kwa safari hii ikiwa ni shindano la Miss Umoja wa Mataifa 2011 (Miss United Nation 2011) limepangwa kufanyika Desemba mwaka huu, Tanzania itakuwa ikiadhimisha miaka 50 ya uhuru.
Shindano warembo 120 kutoka nchi 120 duniani na litaonyeshwa moja kwa moja toka Tanzania katika vituo mbalimbali huku zaidi ya wageni 705 kutoka nje wanatarajiwa kuwepo nchini kwa ajili ya shindano hilo.
Alisema ujio wa wageni hao, hali ambayo itachangia fursa ya kiuchumi ikiwemo utalii, pia alitoa wito kwa makampuni ya Tanzania kujitokeza kudhamini fainali hizo za dunia ili kupata fursa ya kujitangaza kimataifa, Tanzania katika fainali hizo itawakilishwa na Miss Utalii Tanzania 2011, Adelqueen Njozi.

No comments:

Post a Comment

here u,re comments/acha ujumbe wako hapa