Monday, April 4, 2011

Wachezaji wa Judo kuwasili Dar




WACHEZAJI  wanne wa mchezo wa Judo waliokuwa nchini Japan wanatarajia kutua jijini Dar es Salaam , Aprili 4 kwa shirika la ndege ya Misri.
 
Katika taarifa iliyotolewa leo  kwenye  vyombo vya habari na Rais wa mchezo huo Visiwani Zanzibar, Tsuyoshi Shimaoka alisema kuwa  wachezaji hao watawasili majira ya asubuhi ya Aprili 4,  kisha watapata wasaha  wa kuzungumza na vyombo vya habari kwenye  Hoteli ya Kibodia iliyopo jirani na mnara wa saa (Clock tower).
 
Shimaoka aliwataka wadau wa mchezo huo  waliombwa kufika katika hoteli hiyo na kubadilishana nao mawazo ikiwemo kufanya nao mahojiano maalum ambapo watakuwa kuanzia asubuhi hadi saa tisa mchana na baada yha hapo wataondoka kuelekea Zanzibar kwa boti maalum.
 
“Tunaomba wadau wa Judo kufika kwa wingi ilikuweza kujua zaidi kutoka kwa wanamichezo wetu walichojifunza nchini Japan kwa muda wa miezi mitatu, ni hakika italeta changamoto” alisema Shimaoka.
 
Shimaoka aliwataja wachezaji hao kuwa ni pamoja na  Lawa Henry  (Nahodha), Abdalla  Alawi, Khamsi    Hussein  na  Abeid  Dola.
 
Wachezaji hao waliondoka nchini mapema Januari 3, mwaka huu na kwenda nchini humo kujifunza mchezo wa Judo kwenye mji wa Chiba , Japan na kuweza kujiandaa kwa maandalizi ya michezo mbalimbali ya Afrika.
 
Aidha, mbali ya kutokea hali ya matetemeko na Tsunami, wakati wapo huko waliendelea na mafunzo yao hayo kwenye ya kila siku kwenye chuo cha Juntendo na kupata uzoefu wa kutosha ikiwemo kuongeza maalifa katika mapambano ya kitaifa.
  

No comments:

Post a Comment

here u,re comments/acha ujumbe wako hapa