Monday, April 4, 2011

Judo walejea na matumaini


Judo walejea na matumaini 

Na Andrew Chale

 

WACHEZAJI wa mchezo wa judo  waliokuwa mafunzo ya nchini Japani wamerejea na matumaini makubwa ikiwemo kunyakuwa medali katika michezo ya All Africa Game itakayofanyika Septemba mwaka huu.

 

Akizungumz na waandishi wa habari mapema leo asubuhi  Rais wa Chama cha Judo Zanzibar (ZJA), Tsuyoshi Shimaoka,  alisema kuwa wachezaji hao waliwasili mapema asubuhi hiyo wakitokea nchini Japani kwa mafunzo ya mchezo huo

 

waliodumu kwa miezi mitatu, alisema kuwa watahakikisha wananyakuwa kwenye michuano ya 'East Afrika Judo Championship mwezi Julai na wa 'AllAfrica Game' Septemba mwaka huu.

 

"Wachezaji wote wamerudi salama na wameweza kupata mafunzo ya hali ya juu kwenye vyuo mbalimbali vya kimataifa vya Japani vinavyofundisha judo, hivyo nguvu zetu tunazielekeza huko ilikuleta heshima na changamoto kwa nchi za Afrika Mashariki na Afrika kwa ujumla" alisema Shimaoka.

 

Kwa upande wao wachezaji hao Lawa Shauri ambaye ni nahodha wa msafara huo alisema kuwa mafunzo hayo yameweza kuwasaidia ikiwemo kujiimalisha katika mchezo huo na watahakikisha wanakuwa kioo kwa wengine sambamba na kushinda katika michezo iliyopo mbele yao .

 

"Tunashukuru kwenda na kurudi salama, hivyo tunawahakikishia mafunzo tuliopata kule ni ya ushindi na wote tumedhamiria kunyakua medali zote zilizo mbele yetu zaidi tunaiomba Serikali kusaidia mchezo huu" alisema Lawa.

 

Wachezaji hao waliondoka jijini Dar es Salaam Januari 3 na kufikia katika mji wa Chiba  na kupata mafunzo yao kwenye chuo cha kimataifa cha Juntendo.

 

Wachezaji hao ni pamoja na nahodha Lawa Shauri Henry, Abdallah Abdulsamad Alawi, Khamis Azzan Hussein na Abeid Omar Dola.

 

Aidha, Shimaoka alisema kuwa safari za kupeleka wachezaji nchini Japani ni utaratibu uliopo  ambapo awali wanamichezo wa mchezo huo walisha kwenda na kupata mafunzo hivyo kufanya mpaka sasa kupeleka mara nne na kwenye nchi hiyo inayoongoza kwa ubora wa namba moja wa mchezo wa Judo Duniani huku Ufaransa, Korea,China na nchi nyingine zikifuatia.

 

Mwisho.


No comments:

Post a Comment

here u,re comments/acha ujumbe wako hapa