JENERALI Mstaafu wa jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), George Waitara ametoa wito kwa watanzania kuwa na mazoea ya kutembelea na kuupanda mlima Kilimanjaro ambao ndiyo mrefu barani Afrika ilikuongeza chachi ya kiuchumi.
Waitara aliyasema hayo jijini Dar es Salaam, jana katika ukumbi wa uwanja wa Golf wa Lugalo, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari juu ya JWTZ kupanda mlima huo kwa mwaka 2010, ambapo siku ya Desemba 9 wapandaji wakiongozwa na Waitara watakuwa kwenye kilele cha mlima paolipowekwa mwenge wa Uhuru.
"Kwa mwaka huu 2010, kwa kushirikiana na timu maalum tutapanda hadi kilele cha mlima Kilimanjaro ilikutoa hamasa na kuenzi juhudi za waliotangulia kama ilivyokuwa kwa mara ya kwanza kwa kupanda kilele hicho na wananjeshi waliopewa heshima wakiongozwa na Kapteni Alex Nyirenda wa Tanganyika Rifles na kuwasha mwenge" alisema Waitara.
Katika taratibu hizo za JWTZ kupanda mlima huo zilianza rasmi mwaka 2008, na utakuwa endelevu kila mwaka ilikuingeza chachu ya kimaendeleo na kupata kujitanga zaidi ilikuvutia wahisani walio ndani na nje kujitokeza na kusaidia maboresho ya utalii na kuongeza uchumi kupitia mlima hio.
"Lengo la kuwa na taratibu za kupanda mlima huu ni kutangaa fursa zilizopo nchini ili wangine wajifunze kwetu na kutamani kuja kuungana nasi pia kutoa hamasa kwa watanzania waliopo ndani kushiriki na kuwa na taratibu za kuupanda mara kwa mara" alisema Waitara.
Aidha, alisema kuwa, JWTZ limekuwa na na utamaduni wa kupanda mlima huo kama sehemu ya mafunzo yao tangu kipindi cha Uhuru, huku Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi wa kwanza nchini, Jenerali Mrisho Sarakikya(mstaafu) alikuwa na utamaduni wa kupanda mlima huo kila mwaka, jambo linaloendelea kutangaza mlima huo.
"Jenerali Sarakikya kwa kipindi chake alichokuwa akitumikia jeshi na uongozi mbalimbali ameweza kupanda mlima huo mara 47, mpaka alipoamua kupumzika hivyo tunataka kuwatia moyo watu mbalimbali kuwa mstari wa mbele kuonyesha mfano na kupanda mlima huo maalufu Afrika na duniani kote" alimalizia Waitara.
Waitara pia aliwataja wadhamini watakao fanikisha shughuli hizo kuwa ni pamoja na kampuni ya KJ Traders, Serengeti Breweries, Bodi ya Utalii pamoja na Wizara ya Maliasili na Utalii, pia aliwaomba wadau wengine kujitokeza kwani milango ipo wazi ilikuongeza chachu na hamasa zaidi na litakuwa ni la kila mwaka.
Mwisho.
1 comment:
hii ni kweli kabisa watanzania tubadilike tunasubiri mpaka mzungu aje kutuhakazisha juu ya kwenda kuangalia vivutio vyetu mwenyewe hii ni aibu,
kwa nafasi hii napenda kuwapa shavu kituo cha clouds kwa kuwa na kipindi kizuri cha kambi popote kikiwa kinaonyesha uhalisi wa mtanzania halisi
ahsanteni kazi njema
Post a Comment
here u,re comments/acha ujumbe wako hapa