Thursday, November 18, 2010


Mwenyekiti Chipukizi na Mwanaharakti ampongeza Pinda

 

MWENYEKITI wa Chipukizi wa Wilaya ya Kinondoni na Mwanaharakati wa kutetea haki za watoto nchini, Nimka Lameck, amepongeza   Waziri Mkuu Mteule, Mizengo Pinda, kwa kuchaguliwa kwa awamu ya pili  katika nafasi  hiyo.

Nimka alitoa pongezi hizo mapema leo jijini Dar es Salaam alipokuwa akitoa maoni yake juu ya  uteuzi wa waziri mkuu na anaamini atakuwa chachu ya maendeleo nchini hasa katika masuala ya watoto.

"Watoto nchini tunataka mabadiliko ya kweli, hivyo ni hakika Pinda ni chaguo sahihi na tunampongeza kwa hilo , kwani hata kazi yake awamu ya kwanza ya nafasi yake hiyo imeonekana hasa kwa watu walio kwenye makundi maalumu ikiwamo walemavu wa ngozi," alisema Nimka.

 

Alisema licha ya kuonyesha ujasiri huo ambao ulipelekea kumwaga chozi bungeni, kimeleta faraja kwa watu wa makundi yote ikiwemo watoto ambao nao wanafanyiwa vitendo vya kikatili.

Aidha, alishahuri juu ya baraza jipya la mawaziri kuakikisha linatilia maanani hali za watoto nchini ili kuwa na muongozo imara.

"Watoto siku zote tunasahuriwa, hivyo tunataka mawaziri kuwa mstari wa mbele kuhakikisha wanatutimizia haki zetu kuliko ilivyo sasa," alisema Nimka.

 Baadhi ya mambo ambayo walipendekeza kwa wizara mpya kuyafuata ni pamoja na kusimamia haki za watoto kwa ukamilifu ilikuzuia  hali ya mateso wanayokumbana nayo kwa jamii.


"Tunataka jamii iwekwe wazi juu ya haki zetu na mienendo sahihi ya haki na wajibu wa watoto ilikuwa kwenye matumaini ya kuishi kama watoto wengine" alisema Nimka.

Mwisho



No comments:

Post a Comment

here u,re comments/acha ujumbe wako hapa