Thursday, September 2, 2010

Daud Tairo Michael


                                           Daud Tairo Michael
               Kutoka Udereva teksi hadi msanii na mwandaaji wa filamu
                *Anatingisha na filamu za 'Fake Pregnant' Where Is Love, na sasa 'Aunt Suzzy'.




WASANII nchini wataneemeka na kufaidi matunda ya kazi zao za filamu nchini ni pale tu watakapoamua kutoa kazi zilizo na ubora, utashi kwa jamii ikiwemo kufikisha ujumbe wa haraka na mpangilio sahihi wa filamu yenyewe.

Hayo ni maneno yake msanii na mwandaaji wa filamu anayekuja kwa kasi kubwa hapa nchini,  Daud Michael, anayetamba na filamu za ' Upside  Down', 'Where Is Love',  'Fake Pregnant' na filamu ambayo ipo mbioni kutoka iliyojaa mastaa kibao ya 'Aunt Suzzy'.

Katika mahojiano  maalum na  Tanzania Daima Wikienda, Daud Michael  anayemiliki studio yake ya kisasa ijushughulishayo na uandaaji wa filamu mbalimbali hapa nchini inayofahamika kama 'D Production, iliyopo maskani ya Mabibo Makutano  jijini Dar es Salaam.

Daud anasema kuwa mpaka alipofikia ni safari ndefu katika tasnia hiyo ya sanaa kwani aliweza kupita milima na mabonde kama wasemavyo waswahili mpaka kufika hapo alipo na kuwa na kampuni yake hiyo sambamba na kutoa filamu zake ambazo jamii wamezikubali.

Alipotokea Daud!!

Daud alizaliwa mwaka 1984 Mkoani Tanga katika Wilaya ya Kologwe, ambapo kwa mama yake ni mtoto wa pekee jhuku kwa baba yake ni wa tatu. Aliweza kujiunga na elimuya msingi katika shule ya Msingi Msasani na kisha akamalizia elimu yake katika shule ya Sinza.

Aliweza kubahatika kujiunga kusoma shule ya sekondari ya Sinza ambapo aliweza kusoma hadi kidato cha tatu..kufuatia kupata matatizo ya kifamilia ambayo yalikuwa nje ya uwezo wake aliachana na shule na kujiingiza na maswala ya ufundi makanika(gereji).

Daud anasema baada ya kukaa kwa muda aliweza kujifunza udereva ambapo alikuwa akijishughulisha na udereva wa Teksi huko maeneo ya Mabibo. "Unajua kadili siku hali ilivyokuwa inaendelea katika maisha yangu nilikuwa na shahuku ya kuona nafanya kitu kikubwa zaidi ususani katika maswala ya sanaa' anasema Daud.

Hata hivyo kutokana alikuwa na kipaji tokea akiwa yupo shule, ambapo alikuwa anasikia wivu jinsi filamu za kitanzania zinavyoendelea huku zingine zikishindwa kufanya vizuri ikiwemo kufikisha ujumbe.

'Nilikuwa na kaa nikitazama hizi filamu na kukosoa baadhi ya mambo, lakini kwa kuwa ninakipaji niliamua kujiunga na kundi la sanaa ilikuongeza ujuzi zaidi' anasema Daud.
Aliamua kujiunga na kundi la Bahari Artist Group lililokuwa chini ya mwalimu  Joseph Mwasa na Jafari Makatu  hiyo ni mwanzoni mwa mwaka 2007, ambapo aiweza kujifunza mbinu mbalimbali za uigizaji pamoja na kutunga stori ikiwemo kuandaa 'script'.

'Chini ya walimu wa kundi la Bahari, niliweza kuonyesha uwezo wangu wa sanaa kutoka moyoni ambapo weza kudhihirisha uwezo' anasema Daud.

Daud aliweza kukaa na k undi hilo kwa kipindi  kisha aliamua kujitegemea katika filamu ikiwemo kushirikishwa katika baadhi ya filamu  mbazo zinafikia zaidi ya nane.

Kati ya fimu hizo ni pamoja na filamu ya  'My Blood-part two' akiwa kama 'main kalakta' kinara wa filamu namba mbili alitumia jina la Maliki.

Kisha aliwez kuwamo kwene filamu ya 'Money Desire', filamu ya 'Its too lets na filamu nyingine nyingi. "Baada ya kufanikiwa kuwika ndani ya filamu hizo, niamua kuanzisha studio yangu ya maswala ya kuandaa filamu nchini' anasema Daud.

Kwa kuzingatia ubora aliyoupata kutoka kwa kundi lake la zamani pamoja na filamu alizoigiza akiwa ameshirikishwa na kuona anauwezo mkubwa aliamua kuanzisha studio yake hiyo ya D.Production na kufanikiwa kutoa filamu yake ya kwanza ya 'Up side Down' ambayo aliweza kuiigiza kwa ustadi mkubwa na kuweza kukubalika na wadau wengi wa filamu nchini.

"Katika filamu ya Upside Down, ni kati ya filamu ilinipa shida sana kwani niliitajika kuigiza kama chizi nikiwa kati kati ya jalala kuu la kigogo lakini nilifanikiwa na kweli jamii ilikubali' anasema.

Anasema kuwa filamu nyingine iliyompashida shida na taabu sana kuicheza ni ile ya 'Its too late, ' filamu hii niliigiza nabaka …kazi iliyonipa shida sana lakini ndiyo sana niamua kuiumudu' anasema Daud.

Akielezea juu ya Production yake hiyo anasema ameweza kufanikiwa kutoa filamu nne huku filamu za 'Up side Down, Where Is Love na Fake Pregnant zikiwa zipo sokoni  na ya nne ambayo ni 'Aunt Suzzy' inayotalajia kutoka muda wowote kuanzia sasa.

Akielezea filamu ya Fake Pregnant, ambayo imewza kuwa gumzo mitaani, anasema aliumiza kichwa sana kuiandaa ambapo ikielezea juu  familia tajili ambayo kaka wawili mama yao anawataka wampatie mjukuu huku wapenzi wao wanasoma, hivyo wanajikuta wanaangukia kwa mchumba mmoja bila wao kujijua ambaye awali alikua ni kahaba na kuachana na kazi hiyo na kujiingiza katika nguvu za giza.

 "Ni filamu ambayo inanipa faraja kubwa kwani imeja mafundisho ya hali ya juu hata wadau wameipokea kutokana na simu zao wanazonipigia' anasema Daud.

Ndani ya filamu hiyo inawasanii kama Ester Flavian, Soud Ally, Amina Kibbiki, Ayubu Santana na Mboto.

Akielezea ujio wa filamu yake hiyo nyingine mpya ya 'Aunt Suzzy,   iliyojaa mastaa kadhaa wakiwemo wakongwe  Mzee Magari ,na chipukizi wanaokuja kwa kasi Emmed Hamis 'Ramsey wa Bongo', Ester Flavian, Rent Anthon, Fred Kaguo 'mbisahi real, ASuka Soud, Halima Machiwa 'Aunt Suzzy'  na Daud Michael mwenyewe.

Ndani ya filamu hiyo imejaa visa na mikasa katika matukio ya hatari 'action' mbalimbali katika mapenzi,uharamia na ubabe ambao unapelekea Suzzy kujikuta anaishia kifo.

Malengo yake

Daud anasema anataka kwenda kusomea fani hiyo ya sanaa hususani uandaaji katika vyuo vya nje ya nchi ilikuja kuwa na studio kubwa ya maswala ya filamu hapa nchini.


Soko la filamu la sasa na la awali

Daud anasema soko la filamu kipindi cha  sasa limekuwa sana, kulikotokana na kuongezeka kwa filamu nyingi sokoni ambazo zinazalishwa kila kukicha na wandaaji ambao wanataka kuona mara zote filamu  zinaingia sokoni hali hiyo ni tofauti kabisa na kipindi cha nyumba ambacho  tulikua tukishuhudia filamu moja ikitamba sokoni kwa zaidi ya miaka mwili hadi mitatu.

"Kutoa filamu mfululizo ni sawa na mangi anapouza duka, hivyo kama tunaamua kutoa filamu hizo mfululizo ni jambo zuri lakini tuzingatie ujumbe,mpangilio  na maadili ya filamu yenyewe kutokana na maisha yetu halisi pasipo kuiga wangine' anasema Daud.

Akifafanua zaidi, Daud anasema kuwa  tulipotoka katika filamu kipindi cha nyuma, ambapo filamu ilikuwa ikikaa kwa muda mrefu 'madairekta' walikuwa wakifikilia soko na jinsi ya kurudisha fedha zao na pia kujiimalisha katika kutunga ujumbe pasipo kuiga kwenye filamu za nje ikiwemo Naigeria.

Akielezea juu ya wasanii wengi wa zamani ambao sasa hawawiki na baadala yake soko limevamiwa na wasanii wapya 'chipukizi' anasema kuwa wandaaji wa zamani walikuwa wakipitia njia ya mkato kwa kuwachukua wasanii waliokuwa wakigiza katika vipindi vya luninga na kuacha wasanii waliokuwa na uwezo.



"Unajua zamani kulikuwa ni vituko sana , utakuta sisi wasanii 'wachanga' tulikuwa atusaminiki na matokeo yake walikuwa wakichukuliwa wasanii ambao walionekana katika michezo ya kuigiza katika vituo vya luninga na kutunyima fursa sisi wa chini, iliumiza sana wasanii waliokuwa na moyo' anasema Daud

Sasa hakuna wasanii zaidi ya wandaaji wengi kukimbilia kuchukua watu ambao wanamajina katika jamii na kuwapangia  'scene' kwa siki mbili tu anaigiza hii imeweza kuwavunja nguvu wasanii wengi walio na kipaji ambapo wanaona wanatengwa na tasnia hii.

"Kama unasura nzuri ama unauwezo basi ni muda wa kuingia chuo na kusomea sanaa kuliko kuingia katika soko la filamu na kufanya ubabaishaji' anamalizia Daud.


Mwisho

No comments:

Post a Comment

here u,re comments/acha ujumbe wako hapa