Saturday, August 14, 2010

VIJANA TUSIWE MITAJI YA WAGOMBEA, TUSEME BASI

press note; kwa vyombo vya habari.
 
NB; magazeti,blog na redio
asanten
 

'Vijana tuseme basi..tusiwe mitaji  ya wagombea uongozi'

 

Na Mwandishi Wetu

 

VIJANA wameaswa kuepuka kurubuniwa na vitu vidogo kwa kipindi hichi cha kuelekea uchaguazi mkuu na baadala yake wajihadhari ili kuepuka kutumiwa vibaya sambamba na kugeuzwa mitaji ya viongozi.

 

Hayo yalisema jana jijini Dar es Salaam, na mwenyekiti wa muda wa Kata ya Magomeni kwa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Andrew Chale  wakati wa kupitisha  maadhimio,kuziba nafasi zilizokua wazi pamoja na mikakati ya kampeni kwa ngazi ya udiwani wa Kata hiyo zitakazotalajia kuanza Agost 20 mwaka huu

 

Chale ambaye ni mwandishi wa habari wa gazeti la Taznzania Daima na mwanaharakati wa kutetea haki za vijana na watoto waishio katika mazingira magumu, aliwaomba vijana kuacha kutumiwa na viongozi wanaowafuata kipindi hichi na kuwahidi kuwasaidia tokea miaka mitano awajaonekana.

 

"Jamani vijana wenzangu wa magomeni na wa tanzania huu sasa ni wakati wa kusema basi tusiwe jalala la wanasiasa,wakiwapa pesa kuleni siri yenu ipo ..chadema kipe kura yako ilikuweza kuleta mabadiliko ya kweli' alisema Chale.

 

Aidha, aliwataka vijana kutokubaliana na sera za viongozi juu ya kuwapatia ajira kwani kila miaka wanasema hayo na hakuna kipya; Nawaomba vijana wenzangu kwa muda mwingi viongozi tunaowachagua wanatumia migongo yetu kujinufaisha huku wahusika tukiwa hatuna thamani tukatae kugeuzwa mitaji'

 

Katika mkutano huo uliodhuriwa na wajumbe mbalimbali wa chadema kata hiyo ambapo Chale alichaguliwa kushika nafasi hiyo kwa muda wa siku 72 muda ambao utafanyika uchaguzi wa viongozi ndani ya Kata hiyo,

 

Awali nafasi hiyo ya mwenyekiti ilikua ikishikiliwa na Said Omary Said 'Afsa' ambaye kwa sasa anawania udiwani katika Kata hiyo.

 

Kwa upande wake Mwenyeki wa Vijana wa Kata hiyo, Abdalah Mtundu aliwataka vijana kuchagua chama makini na kukipa kura ilikuweza kuendeleza demokrasia nchini.

 

"Umefika wakati wa kila kijana kujitambua ilikujiongezea upeo na maalifa,ni kwa kuichagua chadema pekee' alisema Mtundu.

 

Mwisho

 

 





No comments:

Post a Comment

here u,re comments/acha ujumbe wako hapa