Saturday, August 28, 2010

NEW HOPE FAMILY STREET CHILDREN



 NEW HOPE FAMILY STREET CHILDREN!!
             WANAOMBA MSAADA WAKO WA HALI NA MALI 


UMOJA wa watoto waishio katika mazingira magumu na hatarishi mitaani jijini Dar es Salaam wanaojulikana  (New Hope Family Street Children) wanaomba misaada ya hali na mali ilikuondokana na manyanyaso wanayokumbana nayo mitaani.

Wakiongea na MAFIA BLOG walisema kuwa wanahitaji msaada wa haraka ikiwemo magodoro,vitanda,mashuka na pamoja na vitu vya ndani kufuatia kupata nyumba nzima ya kupanga huko maeneo ya Kigamboni.

Mwenyekiti wa Umoja huo, Omary Raujabu alisema kuwa wanajisikia faraja kwa sasa katika hatua waliofikia ambapo wapo katika taratibu za mwisho kulipiwa kodi ya mwaka nzima ili kuendesha maisha yao kama watu wengine.kodi hiyo wanayotarajiwa kulipiwa ni kiasi cha shilingi Milioni moja na laki mbili.

"Tunaomba wadau waendelee kujitokeza kwa wingi ili kufanikisha maombi yetu kwani tulipofikia sasa ni pazuri hivyo tunaomba misaada zaidi vikiwemo vitu vya ndani chakula' alisema Omary.

Kwa upande wake Katibu wa umoja huo,Hashimu Yusuph alisema kuwa umefika wakati wa kupewa nafasi kwa jamii isiyojiweza ilikukizi maisha ya kila siku kama familia nyingine.

"Sisi tupo mitaani zaidi ya miaka 12, kumepitia shida nyingi hivyo kipindi hiki tumefanikiwa kuwa na umoja wetu ilikusaidiana tunaomba wadau kujitokeza ilikutusaidia mahitaji mbalimbali yakiwemo ya elimu,ajira misaada ya kila siku' alisema Hashimu.

Naye mmoja wa watoto aliyewakilisha wenzake, alisema kuwa  shida wanazozipata ni nyingi hivyo wanaomba misaada ya haraka ilikuweza kuishi kama wengine. "Kurudi nyumbani ni vigumu kwani ni muda mrefu niliondoka miaka 5 iliyopita nimepasahau na wao wamenisahau' alisema John William.

New Hope Family ilianzishwa na umoja wa watoto hao waishio mitaani tokea 2007, huku wakijishughulisha na maswala ya kusaidiana ikiwemo afya,ulinzi  na chakula,walidai kuwa kuanzisha umoja huo ni baada ya kuona watoto wenzao wengi wakinyanyasika ikiwemo kutoka kwa wakubwa zao ambao wanakuwa nao mitaani na wananchi.

Mratibu na msemaji mkuuu wa umoja huo wa New Hope Family Street Children, Andrew Chale  alisema kuwa mpaka sasa wanajisikia faraja kuwa pamoja kwani awali maisha yao yalikua hatarini ikiwemo kunyanyaswa na wananchi mitaani.

"Tunashukuru umoja huu kwani ni hakika baadhi ya watoto na vijana wanaopatwa na mateso mitaani kupungua, kwani pindi watakapo kuwa pamoja wataweza kupata fursa nyingi walizokosa awali zikiwemo za lishe,malazi na ulinzi' alisema Andrew

Akielezea hali ya watoto hao wanayokumbana nayo mitaani, Andrew Chale alisema kuwa awali yeye alipitia maisha kama hayo miaka 10 iliyopita ambapo alikaa mitaani kwa kipindi cha miaka 6, ambapo sasa ameweza kutoka katika hali hiyo na kuishi maisha ya kawaida. "Jamani maisha ya mitaani sio mazuri, ni mateso makubwa kwani unapolala upajui na unapoamka upajui hivyo ukilala barabarani ujue kesho utalala chini ya daraja ama kibaraza cha duka, hii ni mbaya sana , chakula ni hicho cha majalalani ama ukoko' alisema Andrew Chale

Hivyo kwa umoja huo kuwa na nyumba ya kuishi ilikuweza kujikusanya sehemu moja na kufanya mambo ya kijamii lengo lililokua muda mrefu limeweza kutimia kwa sasa ambapo tayari nyumba hiyo iliyopo Kigamboni iliyo na vyumba nane wamekubali kuwapangisha huku kodi ikiwa ni Milioni moja na laki mbili kwa mwaka.

"Misaada wa haraka ni kuweza kuipata pesa hiyo na mahitaji mengine ikiwemo thamani za ndani magodoro,vitanda,vyombo n.k. ilikuweza kujiendesha ndani pindi tutakapoingia humo..

Pia wadau wajitokeze kutusaidia kutusomesha kwa elimu za ngazi zote ikiwemo ya dini,ya kawaida pamoja na mafunzo ya ufundi ikiwemo na kuja kutuajiri ilikujiendesha wenyewe hapo baadae.

Kwa msaada unaweza kuwasiliana na Andrew Chale ama kufika katika ofisi za Tanzania Daima zilizopo mtaa wa Mkwepu jengo la Billicanas gorfa ya kwanza au simu +255719076376/ Omary rajabu; 0657081710


No comments:

Post a Comment

here u,re comments/acha ujumbe wako hapa